Usawiri wa mhusika mlevi katika riwaya teule za Kiswahili
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu ulichunguza Usawiri wa Mhusika Mlevi katika Riwaya Teule za Kiswahili ambazo ni Rosa Mistika (1971), Uwike Usiwike Kutakucha (1978), Ua la Faraja (2004) na Watoto wa Maman’tilie (2012). Utafiti umejadili vyanzo vya mhusika kuwa mlevi wa pombe na athari za mhusika mlevi wa pombe kama ilivyosawiriwa katika riwaya teule za Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa maktabani kwa kusoma na kuchambua riwaya teule za Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Saiko Changanuzi katika uchambuzi wa data. Utafiti huu umebainisha vyanzo vya mhusika kuwa mlevi wa pombe na athari za mhusika mlevi wa pombe kama ilivyosawiriwa katika riwaya teule za Kiswahili. Baadhi ya vyanzo vya mhusika kuwa mlevi wa pombe vinavyobainishwa na riwaya teule ni pamoja na mhusika kutaka ushirika wa kijamii, kutaka kuonekana maarufu au kujulikana katika jamii, kutaka kuondoa mfadhaiko au wasiwasi na kukabiliana na changamoto za maisha. Aidha, athari za mhusika mlevi wa pombe ni kama vile, mhusika mlevi kuwa chanzo cha migogoro, vurugu, usumbufu na kero katika familia, kuiba fedha za mwenzi wake, kufuja fedha, kupoteza ajira, kuathiri mwili, kutelekeza familia, kujiingiza katika tabia hatarishi na kusababisha kifo. Hivyo, utafiti umeweka wazi namna usawiri wa mhusika mlevi katika riwaya teule za Kiswahili unavyolenga kuitahadharisha jamii kuhusu athari hasi za aina mbalimbali zinazosababishwa na ulevi wa pombe kwa mwanajamii mlevi, familia yake na taifa kwa ujumla.