Fasihi simulizi na ukimwi: Mifaano kutoka katika nyimbo za ngoma ya wigashe ya wasukuma
Loading...
Date
2012
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechambua nyimbo za ngoma ya Wigashe. Utafiti ulihusisha nyimbo mbalimbaliza ngoma ya Wigashe zinazohusu UKIMWI. Lengo katika utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza usawiri wa ugonjwa wa UKIMWI katika nyimbo za ngoma ya Wagashe
Data na taaarifaa za utafiti huu zimekusanywa kutoka maktabani na uwandani, na mbinu zilizotumika katika kutupatia data ni mbinu za uchambuzi matini, mbinu ya mahojiano pamoja na majadiliano ya vikundi amabzo zilitupatia data za msingi na data za upili.
katika utafiti wetu zimetumika nyimbo nane na uchunguzi wa nyimbo hizo umefanyika kwa kutumiua mkabala wa kimaelezo kwa kuongozwa na nadharia ya Usosholojia. Baada ya uchambuzi wa nyimbo hizo imebainika kuwa dhamira katika nyimbo hizo zinaujadili ugonjwa wa UKIMWI kwa namna mbalimbali. Kuna dhamira zinazohusu sababu za maabukizi, dalili za UKIMWI, ushauri na uhamasishaji juu ya ugonjwa huu na zile zinazozungumzia juu ya tiba ya UKIMWI. Pia, imedhihirika kuwa ushindani katika nyimbo za ngoma ya Wigashe pamoja na matumizi ya tamadhali za semi vimesaidia kwa kiasi kikubwa katika kuibua dhamira mbalimbali zinazohusu ugojwa wa UKIMWI.
Mwisho, limetolewa hitimisho la utafiti mzima pamoja na mapendekezo ya maeneo ambayo yanahiotaji kutafitiwa zaidi ili kuweza kukuza uelewa wa nafasi ya kazi za fasihi simulizi za kabila la Wasukuma katika kuzungumzia masuala ya kijamii
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8694.S94N96)
Keywords
Sukuma language, Traditional dance, Wigashe, Aids (Disease)
Citation
Nzobe, L.R (2012) Fasihi simulizi na ukimwi: Mifaano kutoka katika nyimbo za ngoma ya wigashe ya wasukuma, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.