(Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1967) Nyerere, Julius Kambarage
Uhuru na Maendeleo ni vitu vinavyohusiana sana;uhusiano wao ni sawa na uhusiano baina ya kuku na yai! Bila ya kuku hupati mayai;na bila mayai kuku watakwisha.Vile vile,bila ya uhuru hupati maendeleo,na bila ya maendeleo ni dhahiri kwamba uhuru wako utaotea.