Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Subject "Bantu"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Ukiushi katika tafsiri ya nyimbo za muziki wa injili kutoka kiswahili kwenda kiingereza(University of Dar es Salaam, 2013) Raphael, HonestUtafiti huu umechunguza Ukiushi katika Tafsiri ya Nyimbo za Muziki wa Injili kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Nyimbo za muziki wa Injili zilizoshughulikiwa ni zile tu zinazoimbwa katika lugha ya Kiswahili na kufanyiwa tafsiri kwenda lugha ya Kiingereza, ambapo maandishi yake huonekana mbele ya kioo cha televisheni, kompyuta au mbele ya pazia la sinema. Utafiti huu umetumia mbinu za kupitia nyaraka mbalimbali, kuchunguza maandiko maktabani, kutumia mbinu ya majadiliano, hojaji na dodoso. Utafiti huu umetumia nadharia tatu mchanganyiko, ambazo ni Nadharia ya Kisemantiki, Nadharia ya Ulinganifu wa Kimuundo na Athari, na Nadharia ya Ulinganifu ya Skopos ambayo huchunguza tafsiri kwa kuangalia ulinganifu wa jambo au kitu kilichopo katika lugha chanzi kiwe sawa katika lugha lengwa. Kuhusu matokeo, imebainika kwamba, tafsiri ya nyimbo nyingi ina ukiushi wa kategoria mbalimbali kama vile ukiushi wa kisemantiki, kimuundo na kimofolojia. Kimsingi, ukiushi huo unasababishwa na wafasiri, ambao wengi wao si mahiri katika taaluma ya tafsiri. Pia, kutokuwa na weledi wa kutosha juu ya lugha zote mbili wanazozishughulikia. Aidha, baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa ili kupunguza ukiushi huo ni pamoja na: Kwanza, kazi zote za tafsiri zifanywe na wataalamu wa tafsiri na siyo mtu yeyote anayejua lugha mbili, yaani zile zinazoshughulikiwa. Hii ni kwa sababu tafsiri ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine; ifahamike kuwa, kuna kanuni na mbinu mbalimbali zinazotumika kufanya tafsiri na si uelewa tu wa lugha zinazoshughulikiwa katika mchakato wa tafsiri.