Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Subject "Babu alipofufuka (2001)"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Dhamana ya wakati kiusimulizi inavyojitokeza katika riwaya ya kiswahili ya kifantansia: uchunguzi kutoka Walenisi (1995) na babu alipofufuka (2001)(University of Dar es Salaam, 2019) Mushi, Anna MichaelUtafiti huu umechunguza dhana ya wakati kiusimulizi katika riwaya ya Kiswahili ya kifantasia. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza jinsi dhana ya wakati inavyojitokeza kiusimulizi katika riwaya ya Kiswahili ya kifantasia. Malengo ya utafiti yalikuwa: Kuonesha aina za wakati kiusimulizi zilizotumiwa na wasanii wa riwaya teule, kubainisha viashiria vya wakati kiusimulizi vilivyotumiwa na wasanii kupitia riwaya teule, na kufafanua dhima ya wakati kiusimulizi katika riwaya ya Kiswahili ya kifantasia. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Naratolojia kwa mujibu wa Genette (1980), atnbapo mihimili ya kipengele cha wakati ilitumika kuchanganua data zilizohusiana na wakati. Ili kufikia malengo hayo, data za utafiti zilipatikana kutokana na uchambuzi wa riwaya teule za Walenisi (1995) na Babu Alipofufuka (2001). Tumebaini kuwa, dhana ya wakati ni nyenzo muhimu katika kusimulia matukio kwa mbinu na viashiria mbalimbali kwani matokeo ya utafiti yameonesha kuwa, riwaya zote mbili zinatumia aina mbalimbali za wakati kiusimulizi . Aina hizi ni pamoja na wakati hadithi, wakati kamili, wakati husishwa na wakati unaotaja muda halisi uliotumika. Aidha, katika lengo la kubainisha viashiria vya wakati, wasanii wametumia viashiria mbalimbali ambavyo ni: giza, nyota, mwezi, pia wametumia viashiria vya maji ya mto, maji ya bomba lililopasuka pamoja na viashiria vya kiwakati kama ballad na mawimbi. Matumizi ya wakati yana dhima mbalimbali kwa mujibu wa utafiti huu. Wakati umeonesha mpangilio wa kazi ya msanii, umetumika kuonesha mtuo, umebainisha udondoshi wa matukio na umeibua mandhari. Pia, wakati umetumika kuelezea vipindi vya historia ya jamii, kufafanua muda maalumu wa matukio, na kutoa muhtasari katika kazi za fasihi. Aidha, wakati umetumika kuonesha hali ya maisha ya wahusika na kudhihirisha mabadiliko mbalimbali chanya ya wahusika kwenye jamii. Mchango wa utafiti huu ni kwamba, umeweka wazi aina za wakati zinazotumiwa na waandishi wa riwaya ya Kiswahili ya kifantasia pamoja na viashiria vya wakati vinavyotumiwa kwenye riwaya hizo, zaidi umechangia kufafanua dhima mbalimbali za matumizi ya wakati katika riwaya ya Kiswahili. Mchango mwingine ni kwamba umeendeleza hoja za wataalamu wengine wanaosema kuwa waandishi hawawezi kuukana wakati katika uandishi wao kwani matukio huhusishwa kwa kutazama majira ya siku hata mwaka. Mtafiti anapendekeza kuwa, kwa sababu utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Naratolojia, utafiti mwingine unaweza kufanyika kwa kutumia nadharia nyingine kama vile Uhalisia iii kuona kama wakati unaoelezwa katika riwaya ya kifantasia unaweza kuhusishwa na hali halisi au la na kueleza dhima yake. Aidha, utafiti mwingine unaweza kufanywa katika kazi nyingine za kifantasia za fasihi andishi ya Kiswahili kama vile tamthilia, hadithi fupi au ushairi andishi iii kujua kama matokeo yatakuwa sawa na matokeo ya utafiti huu na hivyo kutoa hitimisho la jumla la dhana ya wakati kiusimulizi katika kazi za kifantasia za fasihi andishi ya Kiswahili.