Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Subject "Babu Alipofufuka"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Dhima za mhusika mzimu katika riwaya teule za Kiswahili: uchunguzi wa Babu Alipofufuka (2001) na Marimba ya Majaliwa (2008)(University of Dar es Salaam, 2017) Mollell, Rehema DismasUtafiti huu umechunguza dhima za mhusika mzimu katika riwaya teule za Kiswahili, uchunguzi wa Babu Alipofufuka na Marimba ya Majaliwa. Utafiti huu ulichochewa na mawazo ya baadhi ya wataalamu kuonesha kwamba, mizimu haina nafasi yoyote katika jamii ilihali wataalamu wengine wakionesha nafasi na umuhimu wa mizimu katika jamii. Data za utafiti huu zimekusanywa kutoka katika riwaya ya Babu Alipofufuka (Mohamed, 2001) na Marimba ya Majaliwa (Semzaba, 2008). Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uhalisiamazingaombwe pamoja na nadharia ya Ontolojia ya Kibantu. Nadharia ya Uhalisiamazingaombwe ilitumika katika lengo la kwanza lililohusu kubainisha sifa za mhusika mzimu katika riwaya teule za Kiswahili pamoja na lengo la pili ambalo lilikuwa ni kueleza namna mhusika mzimu alivyosawiriwa. Nadharia ya Ontolojia ya Kibantu ilitumika katika lengo la tatu lililohusu kujadili dhima za mhusika mzimu katika riwaya zilizoteuliwa. Utafiti umebaini sifa mbalimbali zilizomtambulisha mhusika mzimu katika riwaya teule kama: kujitokeza kama ndoto, kufanya matendo ya ajabu, kutoa msaada, kutokeza kama sauti ya kicheko, kutokeza katika mazingira ya ajabu, kubadilika sura na umbo. Waandishi wamemsawiri mhusika mzimu akiwa na sifa hizi kwa lengo la kuonya, kuonesha ugumu wa maisha, kukemea ubadhilifu wa mali ya umma unaofanywa na viongozi, kukejeli utamaduni wa nje, kuonesha makazi ya mizimu na kuendana na mazingira aliyomo. Kwa upande mwingine, waandishi wamemsawiri mhusika mzimu kama mpinga ukoloni mamboleo hasa matumizi ya vitu visivyoendana na utamaduni wa Mwafrika kama vile matumizi ya lugha za kigeni kama Kiingereza. Aidha, mzimu amesawiriwa kama mpinga uongozi mbaya hususani viongozi wenye ubinafsi wa kujipendelea wenyewe pasipo kujali wananchi, dhuluma na matumizi ya mabavu kwa lengo la kuwagandamiza wanyonge. Vilevile, mzimu amesawiriwa kama mzalendo katika kuwakumbusha viongozi kutumikia wananchi waliowachagua, mwalimu katika kutoa historia ya matukio mbalimbali yaliyotokea zamani pamoja na utohoaji wa hadithi. Mzimu pia amesawiriwa kama mwenye kujiamini katika kukabiliana na vikwazo pamoja na kutoa msaada kwa wanyonge wanaodhulumiwa ili waweze kupata haki yao. Katika utafiti huu, dhima za mhusika mzimu zilizojitokeza katika riwaya teule ni pamoja na: kukamilisha dhana ya uduara katika kuonesha kwamba kuna kuwapo baada ya kifo, mzimu kama kiumbe cha usamehevu wa makosa kupitia mahusiano ya kidarajia na Mungu, kuonya kwa kukataza mambo yasiyoendana na jamii, kinga ya mabaya pamoja na kutambika.