Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Subject "Asu language"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Majina ya mahali katika jamiilugha ya chasu na maana zake(University of Dar es Salaam, 2014) Yonazi, ElihakiUtafiti huu unahusu majina ya mahali katika jamiilugha ya Chasu na maana zake. Utafiti umeongozwa na nadharia Jumuishi ya Giles ya mwaka 1979. Kwa kutumia mbinu za hojaji, dodoso na mijadala ya vikundi lengwa na kwa usampulishaji usionasibu jumla ya watafitiwa 65 walishiriki, ambapo 35 walikuwa wazee wa umri wa miaka 50 hadi 80 na kundi la pili ni vijana wa miaka 20 hadi 35 ambapo jumla ya vijana 30 walishiriki katika utafiti. Kundi la wazee ndilo lililotuwezesha kupata data thabiti na ya uhakika. Jumla ya majina 97 yalikusanywa kutoka katika kata tano ambazo ni Mhezi, Mshewa, Stesheni, Kisima na Mjini.Katika uchanganuzi wa data matokeo yanaonesha kwamba majina ya mahali katika jamiilugha ya Chasu yana maana. Maana hizo zinatokana na majina ya watu, koo za watu, wanyama, wadudu, miti/mimea. Maana nyingine zimetokana na matukio mbalimbali. Matokeo ya utafiti pia yalionesha kwamba majina katika jamiilugha ya Chasu hayakutolewa kiholela bali vigezo vya kiisimujamii kama vile matukio muhimu na tabia na/ sura ya nchi vilizingatiwa. Vilevile majina mengine ya mahali katika jamii hii yalitolewa kutokana na jamii nyingine zilizokuwa na uhusiano na jamii ya Waasu. Matokeo pia yalionesha kwamba baadhi ya majina ya mahali katika jamiilugha ya Chasu yamebadilika kutoka kipindi kimoja cha kihistoria hadi kingine. Mabadiliko hayo yapo ya aina mbili: mabadliko ya jina zima na mabadiliko ya kimatamshi.