Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Subject "African literature"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item usawiri wa familia pana ya kiafrika: mifano kutoka Riwaya za G. Ruhumbika na C.S. Chachage(University of Dar es Salaam, 2012) Shaabani, AmidaTasnifu hii inachunguza usawiri wa dhana ya familia pana katika riwaya za Kiswahili. Inalenga kuchunguza utokeaji wa dhana ya familia pana ya Kiafrika katika riwaya teule za Ruhumbika ambazo ni Miradi Bubu ya Wazalendo na Janga Sungu la Wazawa pamoja na riwaya teule ya Chachage ambayo ni Makuadi wa Soko Huria.Tasnifu imeshughulikia dhana ya familia pana ya Kiafrika kwa kubaini muundo wa familia hiyo pana, kuonesha uhusiano na majukumu ya wanafamilia na pia kubaini athari za mabadiliko ya kijamii katika familia pana.Aidha kwa kutumia nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika na Mkabala wa Kidhamira mtafiti aliweza kukusanya dhamira zinazohusiana na dhana ya familia pana ya Kiafrika katika riwaya teule na kuziorodhesha, kisha kubaini muundo wa familia pana, uhusiano na majukumu ya wanafamilia katika familia pana na athari za mabadiliko ya kijamii katika familia hiyo.Matokeo ya utafiti wa tasnifu hii yanaonesha kuwa muundo wa familia pana ya Kiafrika uliojitokeza unahusisha wazazi ambao ni baba na mama, babu na bibi, watoto tena wengi wanaozaliwa ndani ya familia pana, watoto na ndugu wengine wanaolelewa hapo, marafiki, waliokufa, watoto ambao hawajazaliwa pamoja na muundo wa familia pana katika kiwango cha jamii.Uhusiano na majukumu ya wanafamilia uliojitokeza ni pamoja na uhusiano baina ya mume na mke, uhusiano wa watoto na ndugu zao ndani ya familia, uhusiano na majukumu baina ya wazazi na watoto wao na wale wanaolelewa hapo pia uhusiano wa wanafamilia katika kiwango cha jamii. Athari za mabadiliko ya kijamii katika familia pana ni ubinafsi, usaliti, suala la utajiri, imani za ushirikina pamoja na tamaa za kimwili ambayo yanaathiri uhusiano na mshikamano wa ndugu na wanafamilia katika familia pana. Mwisho, unatolewa muhtasari wa tasnifu, hitimisho na mapendekezo.