Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Subject "Africa"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Usawiri wa dini ya asili katika kazi za fasihi andishi ya kiswahili mifano kutoka kazi za Kitereza (1980) na Ruhumbika (2001)(University of Dar es Salaam, 2014) Selestine, SeveraUtafiti huu unahusu usawiri wa dini ya asili katika kazi za fasihi andishi ya Kiswahili. Pamoja na ushahidi wa wanazuoni mbalimbali waliotafiti dini ya asili katika muktadha wa kijamii na namna ilivyorithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine kwa njia ya fasihi simulizi, hakuna utafiti ulioangalia kwa kina jinsi dini ya asili ilivyosawiriwa katika kazi za fasihi andishi ya Kiswahili, hususani riwaya. Hivyo, utafiti huu ulikusudia kutafiti usawiri wa dini ya asili kama dhamira katika fasihi andishi ya Kiswahili kwa kutumia mifano kutoka riwaya za Bw. Myombekere na Bi. Bugonoka na Ntulwanalwo na Bulihwali na Janga Sugu la Wazawa. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Ontolojia ya Kibantu kama mwongozo katika uchambuzi wa data msingi zilizopatikana katika riwaya mbili zilizotumika katika utafiti huu. Ili kushadidia dhamira zilizojadiliwa kutoka katika riwaya teule, watu kumi na wanane kutoka katika kabila la Wakerewe walihojiwa. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, dhamira ya dini ya asili imesawiriwa kwa kujengwa na dhamira kuu ya uzazi unaosawiriwa kama ufufuko unaounganisha wafu na walio hai. Dhamira ya uzazi inakamilishwa na dhamira nyingine za kifo na uhai, matambiko, mwonekano wa mizimu na uganga. Dhamira hizi zimesawiriwa zikihusisha kufa kwa mwanadamu na kuzaliwa tena au kufa na kuendelea kuwako katika ulimwengu wa mizimu na mawasiliano kati ya wafu na walio hai. Ndoa imeoneshwa kama hatua muhimu ya chanzo cha uzazi na mwendelezo wa ukoo. Hivyo, utafiti umebaini kuwa usawiri wa dini ya asili katika riwaya teule ulilenga kutoa elimu kuhusu dini ya asili na kuihifadhi kama utambulisho na amali muhimu kwa Waafrika hususani Wakerewe. Utafiti pia umebaini usawiri wa dhamira ya dini ya asili umefanyika katika hali ya kuonesha changamoto zinazoikabidhi, mojawapo ikiwa matumizi ya dini ya asili kama chombo cha kuleta maovu katika jamii hasa inapochanganywa na dini za kigeni kama Ukristo na Uislamu.