Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Subject "Adult education"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Mgongano wa sera ya matumizi ya lugha katika programu za elimu ya watu wazima nchini Tanzania(University of Dar es Salaam, 2014) Ntulo, Kornel EsauUtafiti huu unahusu Mgongano wa Sera ya Matumizi ya Lugha katika Programu za Elimu ya Watu Wazima nchini Tanzania. Utafiti huu ulifanyika katika wilaya ya Makete, mkoa wa Njombe. Utafiti ulihusisha jumla ya watafitiwa 40. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano na hojaji. Utafiti huu umetumia mkabala wa kinadharia wa Upangajilugha unaopendekezwa na mwanaisimujamii Haugen (1966). Kwa kuzingatia matokeo ya utafiti, imebainika kuwa kuna matamko 4 ya Sera ya Lugha na Sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Tanzania yanayogongana. Matamko hayo ya sera ya lugha, yalionekana kuwa na mgongano kwa sababu bado yapo na hakuna sera iliyorekebishwa ili kuondoa mgongano huo. Lengo lingine la utafiti huu lilikuwa ni kujua sababu za mgongano wa sera ya matumizi ya lugha Tanzania unasababishwa na nini. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba kuna sababu nne za msingi zinazofanya kuwe na mgongano. Sababu hizo ni kusita kwa serikali kutofanya maamuzi, mapungufu katika katiba ya nchi, mvutano baina ya wanasiasa na wataalamu na mwisho ni sababu ya utegemezi wa nchi ya Tanzania kutoka nchi zilizoendelea kiuchumi. Kwa kuzingatia matokeo yaliyopatikana kwa njia za hojaji na mahojiano, mgongano huu wa matumizi ya lugha una athari kuu tatu kwa programu za elimu ya watu wazima. Athari hizo ni kuzorota kwa programu za elimu ya watu wazima nchini Tanzania, kupotea kwa fursa za elimu kutokana na ufinyu wa fursa hizo kupitia mfumo rasmi na kukosekana kwa uhalisia wa mafunzo yanayotolewa katika programu za elimu ya watu wazima nchini Tanzania. Inapendekezwa kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iandaliwe kwa kuzingatia Sera ya Utamaduni hasa katika kipengele cha lugha inayofaa kufundishia Elimu ya Watu Wazima nchini Tanzania.