Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Subject ", Bantu language"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Toni katika vitenzi vya kihehe(University of Dar es Salaam,, 2012) Elither, Kindole,Tasinifu hii ni zao la utafiti ulioshughulikia “Toni katika Vitenzi vya Kihehe”. Kwa ujumla ripoti ya utafiti huu imegawanyika katika sehemu kuu tano ambazo tumeziita sura. Sura ya kwanza imeshugulikia utangulizi kwa ujumla ambapo imeangalia kwa ufupi lugha ya Kihehe, tatizo la utafiti, mapitio ya kazi zilizotangulia na kiunzi cha nadharia kilichotumika katika uchanganuzi wa data ambacho ni Fonolojia Vipandesauti Huru. Sehemu hii pia imetoa maelezo ya mbinu na zana zilizotumika kukusanya data. Aidha, tumeeleza mawanda ya utafiti huu katika sehemu hii. Sura ya pili imeangazia vipengele muhimu vya kiisimu vya lugha ya Kihehe, kama vile vitamkwa na michakato ya kifonolojia na michakato ya kimofolojia. Vilevile sehemu hii imejadili mambo ya msingi kuhusu toni ya lugha ya Kihehe: miongoni mwa mambo hayo ni kiinitoni, kiimbo toni msingi, upachikaji wa kiinitoni na toni inayohusishwa na kiinitoni. Sura ya tatu imejikita zaidi katika uchanganuzi wa data, ambao umeeleza ruwaza ya toni katika vitenzi vya lugha hii. Uchanganuzi ulioibua mchango na mawazo mapya ya utafiti. Sura ya nne imetumika kutoa muhtasari wa tasinifu nzima, hitimisho na mapendekezo kwa ajili ya utafiti zaidi.