Kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete alihaidi kuinua hadhi ya hospitali saba nchini na kuzifanya za rufani na zile za rufani kupandishwa kuwa hospitali maalumu kutibu magonjwa yaliyoshindikana katika hospitali za rufani, wakati huo huo mgombea mwenza kupitia NCCR mageuzi Bw. Ali Omar alihaidi kupunguza kansa Zanzibar.