Politics

Permanent URI for this collection

Browse

Recent Submissions

Now showing 1 - 20 of 20
 • Item
  Mchakato wa kampeni na matokeo ya uchaguzi mkuu 2005
  (University of Dar es Salaam, 2005-12-19)
  Magazeti mbalimbali yaliyoandikia mchakato mzima wa uchaguzi na matokeo mwaka 2005. Katika kampeni zake Kikwete alihaidi kupiga vita umasikini . Rais Kikwete alishinda uchaguzi kati ya wagombea 10 kutoka vyama vya siasa ambapo nafasi ya pili ilishikwa na mgombea wa CUF Professa Ibrahim Lipumba alipata kura 1, 317,220 sawa na asilimia 1.61 na mgombea kupitia tiketi ya CHADEMA Freeman Mbowe alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 671.780 sawa na asilimia 5.921, Augustino Mrema wa TLP alishika nafasi ya nne na kupata kura 84.131 bila asilimia hata 1. Vyama vingine ni NCCR Mageuzi (56,438), DP (39,990), NLD (21, 525), PPT-Maendeleo (18.741), Democrasia Makini (17,033) na SAU 16,380).
 • Item
  Matokeo ya uchaguzi November 2005
  (University of Dar es Salaam, 2005-11-30)
  Chama Cha Wananchi (CUF) kilinyakua majimbo yote 18 ya uchaguzi yaliyopo kisiwani Pemba wakati Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kilipata ushindi katika kisiwa cha Unguja.
 • Item
  Kampeni za uchaguzi mkuu
  (University of Dar es Salaam, 2010-09-19)
  Kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete alihaidi kuinua hadhi ya hospitali saba nchini na kuzifanya za rufani na zile za rufani kupandishwa kuwa hospitali maalumu kutibu magonjwa yaliyoshindikana katika hospitali za rufani, wakati huo huo mgombea mwenza kupitia NCCR mageuzi Bw. Ali Omar alihaidi kupunguza kansa Zanzibar.
 • Item
  Uchaguzi mkuu Zanzibar
  (University of Dar es Salaam, 2010-10-05)
  Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 Zanzibar wagombea 19 wa vyama vya siasa hawakurejesha form zao za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika majimbo ya wilaya kisiwani Unguja.
 • Item
  Consititution review
  (University of Dar es Salaam, 2010-12-26)
  Yasemavyo magazeti kuhusu maoni mbalimbali ya marekebisho ya katiba mpya.
 • Item
  Matokeo ya uchaguzi 2005
  (University of Dar es Salaam, 2005-07-18)
  Yasemavyo magazeti kuhusu mchakato wa kampeni na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 5. Uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 walipatikana wagombea wa urais kumi kati ya wagombea 13 wa vyama tofauti akiwemo mwanamama mmoja Anna Senkero kupitia tiketi ya PPT-Maendeleo.
 • Item
  Miaka minne baada ya kifo cha Mwalimu Nyerere
  (University of Dar es Salaam, 2003-10-14)
  Katika kumbukizi za kifo cha baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere alifariki 14.10.1999 katika hospitali ya Saint Thomas, London, Uingereza, mashirika mbalimbali, taasisi binafsi na serikali pamoja na Watanzania wote wanaendelea kumkumbuka kwa mengi katika miaka yote ya utawala wake. Mwalimu aliendelea kua kioo cha uongozi wa umma. Alisisitiza juu ya elimu kama njia ya kuwakomboa watanzania, kuleta uhuru wa Watanzania, kujenga umoja, upendo na mshikamano, kuleta muungano wa Tanganyika na Zanzibar nk.
 • Item
  Serikali ya awamu ya nne na ujambazi
  (University of Dar es Salaam, 2006-01-24)
  Katika uongozi wa awamu ya nne, majambazi waliijaribu na kuitikisa serikali ya Kikwete kwa uporaji na mauaji mbalimbali. Miongoni mwa majambazi hao, walikuwemo vigogo wa jeshi la polisi wakiwemo makamanda wa polisi wa mikoa nao walituhumiwa wa ujambazi.
 • Item
  Kuvunjika kwa Jumuiya ya Africa Mashariki
  (University of Dar es Salaam, 1977-08-05)
  Rais Nyerere alisema kuvunjika kwa Jumuiya ya Africa Mashariki lilikua ni pigo kubwa kwa watanzanikwa sababu kunarudisha nyuma juhudi za ukombozi.
 • Item
  Maadamano ya CUF.
  (University of Dar es Salaam, 2001-01-18)
  Magazeti mbalimbali yaliandika juu ya maadamano ya Chama Cha Wananchi CUF. Chama cha CUF kiliandaa maadamano ya amani yaliopangwa kufanyika kote nchini January 27 kabla ya kumalizika kwa muda wa siku 90 ambazo chama kilitaka uchaguzi wa Zanzibar uwe umerejea na kusema kua endapo uchaguzi hautaitishwa baada ya siku 90 basi kitakuwepo kisasi kwa sababu uchaguzi Zanzibar haukuwa wa huru na haki. Pamoja na Jeshi la police kuzuia maadamano hayo lakini mkuu wa CUF bwana Juma Duni Haji alisema maandamano yao lazima yafanyike January 27 2001
 • Item
  Rashid Mfaume Kawawa 1926-2009
  (University of Dar es Salaam, 2010-01-01)
  Waziri mkuu na makamu wa pili wa Rais mstaafu, mzee Rashid Mfaume kawawa alifariki dunia katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa baada ya afya yake kubadirika ghafla. Mzee Kawawa alikua miongoni mwa wanasiasa na watanzania waliokua nguzo kubwa ya kutete na kuulinda muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mzee Mfaume Kawawa alitumia muda mwingi kuhimiza umoja na mshikamano wa watanzania wakati wa uhai wake. Mzee Kawawa alizikwa nyumbani kwake Madale January 2, 2010.
 • Item
  Taarifa ya tume ya Rais ya uchuguzi wa matukio
  (University of Dar es Salaam, 2001-01-26)
  Tume iliyoundwa chini ya Rais Benjamin Mkapa kufanya uchungunzi kuhusu chanzo, matukio na athari za matukio ya tarehe 26 na 27 January 2001 ilibaini ya kwamba maandamano yalifanyika kabla ya tarehe hizo husika. Katika Uchungunzi uliofanyika ilibainika kwamba sababu na vyanzo vilivyosababisha matukio ya January 26 na 27 ni udhaifu wa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC), uchaguzi haukuwa wa haki na huru, serikali kutoheshimu maamuzi ya wananchi , vyombo vya dola kujiingiza katika siasa nk. Tume iliafiki kuwa yaliyoelezwa ndio vyanzo halisi vya matukio hayo yaliyoleta athari mbalimbali ikiwemo vifo na uharibifu na upotevu wa mali.
 • Item
  Uchaguzi mkuu 2010.
  (Uiversity of Dar es Salaam, 2010-10-01)
  Magazeti mbalimbali yaliandika juu ya uchaguzi mkuu wa ubunge, udiwani na urais mwaka 2010.Wagombea kupitia vyama vyao walitumia kila mbinu kuwashawishi wapiga kura. Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete alimwaga ahadi zake nzito ikiwemo ya kujenga barabara hadi Kigoma yenye urefu wa kilometa 7000. Naye Lipumba alihaidi kujenga kiwanda cha matunda Kagera.
 • Item
  Kifo cha Dk. Omary Ali Juma
  (Uiversity of Dar es Salaam, 2001-07-06)
  Magazeti mbalimbali yaliandika juu ya kifo cha aliyekua makamu wa Rais awamu ya tatu Dk. Omary Ali Juma aliyefariki ghafla kwa mshituko wa moyo na kusababisha kufutwa kwa ziara ya maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam DITF.
 • Item
  Corruption in Tanzania: Killing knife of the national development
  (Uiversity of Dar es Salaam, 2003-01-22)
  Magazeti mbalimbali yaliadika juu ya mjadala aliouzua Dk. Kitine juu ya kushamiri kwa rushwa katika serikali na chama tawala. Mjadala huo ulizuka baada ya Jaji Joseph Warioba kutoa ripoti kuhusu rushwa kutofanyiwa kazi ipasavyo. Naye profesa Lipumba alisema katika mihadhara iliyofanyika nchini Swedeni, tathmini ya sera za maendeleo Tanzania, repoti ya rushwa ya jaji Warioba ilichambuliwa na kubaini kua ripoti hiyo iliwafatilia wala rushwa wadogo (Dagaa) na kuwaacha wala rushwa wakubwa (Papa).
 • Item
  Mauaji Wilayani Kilosa
  (Uiversity of Dar es Salaam, 2000-10-27)
  Watu saba walifariki katika mapigano baina ya wafugaji na wakulima wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Chanzo cha mapigano hayo kilikuwa ni ugomvi baina ya mfugaji mmoja wa jamii ya kimasai kupigwa risasi kichwani na mkulima aliyefahamika kama Hasssan Kirungi. Kabla ya mauaji wafugaji waliwashambulia wakulima na wanakijiji na baadaye kuchoma moto nyumba mbili za mwenyekiti wa kitongoji cha kikenge.
 • Item
  Kuugua hadi kufa kwa baba wa Taifa
  (Uiversity of Dar es Salaam, 1999-10-14)
  Kifo cha baba wa Taifa na Mwasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kilitokea nchini London mnamo tarehe 14/10/1999 saa 4:30 za Africa Mashariki katika hospitali ya Mtakatifu Thomas, London Uingereza alikokua amelazwa. Mwalimu Nyerere aligundulika kua na kansa ya damu . Mwalimu alizikwa nyumbani kwake Mwitonga kijijini Butihama, mkoa wa Mara, Wilayani Musoma.
 • Item
  Cuf disaster: police killing in Zanzibar and Pemba
  (Uiversity of Dar es Salaam, 2001-01-28)
  Eleven people including a policeman were killed in Unguja and Pemba islands in running battles between the police and demonstrators believed to be supportes of the opposition Civil United Front (CUF). In that case, seven people were killed in Pemba and four in Unguja while 35 others were injured.
 • Item
  Utendaji wa serikali awamu ya tano
  (Uiversity of Dar es Salaam, 2015-11-24)
  Magazeti mbalimbali yaelezea utendaji kazi wa Rais awamu ya tano, yaangazia siku 100 za mwanzo za uchapaji kazi wa Rais Magufuli, miongoni mwa mambo aliyohaidi kufanya Rais ni pamoja na kupambana na rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya, kuondoa wafanyakazi hewa serikalini, ukusanyaji mapato na ubanaji matumizi, elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne nk. Yote haya yakiongozwa na kauli mbiu "Hapa Kazi Tu".
 • Item
  Mchakato wa kampeni na matokeo ya uchaguzi mkuu 2005
  (Uiversity of Dar es Salaam, 2005-12-19)
  Magazeti mbalimbali yaliyoandikia mchakato mzima wa uchaguzi na matokeo mwaka 2005. Katika kampeni zake Kikwete alihaidi kupiga vita umasikini . Rais Kikwete alishinda uchaguzi kati ya wagombea 10 kutoka vyama vya siasa ambapo nafasi ya pili ilishikwa na mgombea wa CUF Professa Ibrahim Lipumba alipata kura 1, 317,220 sawa na asilimia 1.61 na mgombea kupitia tiketi ya CHADEMA Freeman Mbowe alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 671.780 sawa na asilimia 5.921, Augustino Mrema wa TLP alishika nafasi ya nne na kupata kura 84.131 bila asilimia hata 1. Vyama vingine ni NCCR Mageuzi (56,438), DP (39,990), NLD (21, 525), PPT-Maendeleo (18.741), Democrasia Makini (17,033) na SAU 16,380).