Kifo cha baba wa Taifa na Mwasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kilitokea nchini London mnamo tarehe 14/10/1999 saa 4:30 za Africa Mashariki katika hospitali ya Mtakatifu Thomas, London Uingereza alikokua amelazwa. Mwalimu Nyerere aligundulika kua na kansa ya damu . Mwalimu alizikwa nyumbani kwake Mwitonga kijijini Butihama, mkoa wa Mara, Wilayani Musoma.