Browsing by Author "Sylivester, Johanes"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Ubadilishaji msimbo bungeni na athari zake kwa wasikilizaji(University of Dar es Salaam, 2011) Sylivester, JohanesWakati takribani 5% ya watanzania ndio wanaofahamu Kiingereza (Msanjila 2004:45 akimnukuu Schmied 1989), hali halisi inaonesha kuwa mijadala ya Bunge inaendeshwa kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Kutokana na hali hii utafiti huu ulihusu ubadilishaji msimbo Bungeni na athari zake kwa wasikilizaji na uliongozwa na modeli ya Bell (1984) “Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji” na mkabala wa Fishman (1971) “Mkabala wa Mawanda”. Kwa kutumia mbinu za hojaji, usaili na mijadala ya vikundi lengani na kwa usampulishaji nasibu tabakishi tuliweza kuwatafiti wasikilizaji 775 kutoka Wilaya za Nyamagana na Magu mkoani Mwanza. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, wastani wa 08.90% tu ya wasikilizaji ndio wanaoelewa kwa kiwango kilichokusudiwa mijadala inayohusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Pili, kwa wasioelewa takribani 59.23% hawatafuti mbinu mbadala za kuelewa mijadala hiyo. Tatu, 81.68% ya watafitiwa hawafurahishwi na uzungumzaji wa namna hii kwani hawapati ujumbe uliokusudiwa na kubadilisha Kiswahili na Kiingereza ni kutokithamini Kiswahili na utamaduni wake. Ili kuondoa athari hasi zinazosababishwa na ubadilishaji msimbo Bungeni, 85.55% ya wasikilizaji wanapendekeza kuwa Kiswahili kiwe lugha pekee na rasmi ya kuendeshea shughuli za Bunge. Hawa wanatoa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa; kinaeleweka kwa watanzania wengi na hivyo kitawezesha usemezano uliosawa kati ya Bunge na wadau wake; ni lugha ya taifa na inafungamana na utamaduni wa watanzania; kinaleta umoja na kuondoa ubaguzi; kinaepusha utumwa wa kifikra; ni lugha rasmi ya Bunge la Afrika na itasaidia kukilinda na kukikuza Kiswahili. Pia, watafitiwa wametoa maoni ya jumla ambayo kimsingi yanalenga kukiimarisha Kiswahili kidhima.Item Uchanganuzi Kilongo wa kauli zenye kutweza au kukweza staha katika mijadala ya bunge la Tanzania(University of Dar es Salaam, 2016) Sylivester, JohanesUtafiti huu unahusu uchanganuzi kilongo wa kauli zenye kutweza au kukweza staha katika mijadala ya BJMT katika kipindi cha mwaka 1980 hadi 2014.Data ilikusanywa kwa mbinu za uchambuzi wa nyaraka, ushuhudiaji, hojaji na usaili na kuchambuliwa na kufasiriwa kwa mkabala wa uchanganuzi kilongo shirikishi na mpishano huru. Walengwa wa utafiti walikuwa Wabunge wa BJ MT. Nadharia iliyotuongoza ni Nadharia ya Staha ya Brown na Levmson (1987) inayodai kuwa , kuna kauli zenye kutweza staha na iii kauli hizo zikweze staha mzungumzaji anatakiwa kuzisuka kwa kutumia mbinu faafu za kistaha. Pia, tulizingatia maboresho ya Fraser (1990) anayedai kuwa ili mzungumzaji akweze staha lazima azungumze kwa kuzingatia kanuni zinazodhibiti majadiliano. Kutokana na uchanganuzi kilongo uliozingatia vipengele vya kinadharia, kanuni za Bunge na muktadha wa mazungumzo data tuliyoipata imetupa vipengele vinavyohusiana na kauli zenye kutweza au kukweza. Miongoni mwa kauli hizo ni matusi, kumshambulia Mbunge kuwa ni mnafiki au sio makini, kusema uongo, kuhamasisha uvunjifu wa sheria, kuonesha kuwa wenzio ni punguani, vichaa au wendawazimu, kujivuna au kubeza wengine, kumpa taarifa Spika (Kiti) au kutotii maelekezo yake, kutotumia neno 'Mheshimiwa' kabla ya jina la Mbunge, kauli za kibaguzi na mwisho kuzungumzia mambo ya siri ya Mbunge. Kwa upande wa kauli zenye kukweza staha, utafiti unaweka wazi kuwa ili zijitokeze ni lazima mzungumzaji ateue mbinu faafu za kistaha zitakazomwezesha kulinda utu wa wasikilizaji pamoja na makatazo yanayodhibiti matumizi ya lugha Bungeni. Mbinu hizo ni pamoja na ubadili haji msimbo, matumizi ya kauli ya kutendwa na kutendana, kunukuu, matumizi ya nafsi ya kwanza wingi, matumizi ya vitambulisho hadhi, uteuzi mzuri wa msamiati, matumizi ya njeo ya wakati uliopita //-Ii-// mahali pa wakati uliopo //-na-// wakati wa kuuliza swali na uepukaji. Kwa ujumla, utafiti umeonesha kuwa, uwepo wa kauli zenye kutweza staha Bungeni unatokana na kutotumia mbinu faafu za ki taha. Matokeo ya utafiti huu yanachangia maarifa mapya katika taaluma ya isimu-tumizi Y . Kiswahili hasa katika taaluma za pragmatiki, isimujamii na elimu-mitindo. Pia, yanachangia katika kipengele cha uchanganuzi kilongo kwa kupendekeza mbinu za uchanganuzi kilongo shirikishi na uchanganuzi kilongo mpishano huru kama mbmu za kuchambua na kufasiri data. Kipekee kabisa, utafiti huu unachambua kwa undani kipengele cha staha ambacho ni cha pragmatiki katika mijadala ya Bunge ili kuweza kupata ruwaza za lugha ya kibunge zenye kukweza staha. Ili kubainisha ruwaza za lugha ya kibunge tunapendekeza utafiti zaidi utakaobainisha vipengele vya kiisimu vinavyounda lugha hiyo. Pia, kuhusu mbinu za kistaha katika lugha ya Kiswahili kwa ujumla , tupendekeza tafiti nyingine kufanyika kwenye taasisi nyingine pia na katika mazmgua yasiyo rasmi.