Ubadilishaji msimbo bungeni na athari zake kwa wasikilizaji

No Thumbnail Available
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Wakati takribani 5% ya watanzania ndio wanaofahamu Kiingereza (Msanjila 2004:45 akimnukuu Schmied 1989), hali halisi inaonesha kuwa mijadala ya Bunge inaendeshwa kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Kutokana na hali hii utafiti huu ulihusu ubadilishaji msimbo Bungeni na athari zake kwa wasikilizaji na uliongozwa na modeli ya Bell (1984) “Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji” na mkabala wa Fishman (1971) “Mkabala wa Mawanda”. Kwa kutumia mbinu za hojaji, usaili na mijadala ya vikundi lengani na kwa usampulishaji nasibu tabakishi tuliweza kuwatafiti wasikilizaji 775 kutoka Wilaya za Nyamagana na Magu mkoani Mwanza. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, wastani wa 08.90% tu ya wasikilizaji ndio wanaoelewa kwa kiwango kilichokusudiwa mijadala inayohusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Pili, kwa wasioelewa takribani 59.23% hawatafuti mbinu mbadala za kuelewa mijadala hiyo. Tatu, 81.68% ya watafitiwa hawafurahishwi na uzungumzaji wa namna hii kwani hawapati ujumbe uliokusudiwa na kubadilisha Kiswahili na Kiingereza ni kutokithamini Kiswahili na utamaduni wake. Ili kuondoa athari hasi zinazosababishwa na ubadilishaji msimbo Bungeni, 85.55% ya wasikilizaji wanapendekeza kuwa Kiswahili kiwe lugha pekee na rasmi ya kuendeshea shughuli za Bunge. Hawa wanatoa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa; kinaeleweka kwa watanzania wengi na hivyo kitawezesha usemezano uliosawa kati ya Bunge na wadau wake; ni lugha ya taifa na inafungamana na utamaduni wa watanzania; kinaleta umoja na kuondoa ubaguzi; kinaepusha utumwa wa kifikra; ni lugha rasmi ya Bunge la Afrika na itasaidia kukilinda na kukikuza Kiswahili. Pia, watafitiwa wametoa maoni ya jumla ambayo kimsingi yanalenga kukiimarisha Kiswahili kidhima.
Description
Available in print form
Keywords
Swahilii language, English language, Parliaments, Tanzania
Citation
Sylivester, J (2011) Ubadilishaji msimbo bungeni na athari zake kwa wasikilizaji master dissertation, University of Dar es Salaam, Available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx?parentpriref=