Browsing by Author "Robert, Shaaban"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Koja la lugha(Oxford University Press, 1969) Robert, ShaabanKwa asili shairi hili liliandikwa na Francois Marie Arouet de Voltaire aliyeishi zamani za 1694-1778, Karne mbili na nusu zilizopita. Huyu ni mmoja wa walimu wakuu na mwandishi bora kabisa wa kifaransa.Kwa tafsiri ya kiingeleza iliyofanywa na Joseph McCabe shairi hili lilipangwa kwa beti kumi za mistari 234.Kwa tafsiri ya kiswahili limeandikwa na nguli Shaaban Robert na kupangwa kwa beti 48 za mistari 240,kila ubeti mistari mitano. Usanifu wa shairi hili wapendeza na kufikirisha sana.Item Kufikirika(Mkuki na Nyota, 1967) Robert, ShaabanKUFIKIRIKA ni nchi moja kubwa katika nchi za dunia,Kaskazini imepakana na Nchi za Anasa,Kusini nchi ya majaribu,Mashariki Bahari ya kufaulu na magharibi safu ya milima ya jitihadi.Ramani ya nchi hiyo ni adimu kupatikana kwasababu nchi yenyewe haiandikiki ila hufikirika kwa mawazo tu.Njia ya kwenda nchi hiyo hukanyagwa kwa fikira siyo nyayo.Wafikirika wengi nao ni wazazi mno, nyumba ina watoto wanane hata kumi na sita si jambo la ajabu.Jumla ya wafikikirika ni sawa na nusu moja ya makabila yote duniani. ina ufalme mkubwa kuliko falme zote za mataifa mengine,Raha inayopatikana katika nchi yakufikirika ni kama kama ile iliyo katka pepo, isipokuwa katika kufikirika kuna maradhi na mauti lakini katika pepo kuna uzima na maisha ya milele.Nchi hiyo ilitawaliwa na nasaba kubwa sana ya wafalme ambao waliungana kwa viungo vyao kama mkufu, lakini mfalme wa mwisho alichelewa kupata mtoto wa kumrithi. kitabu hiki kinasimulia habari ya mfalme huyo