Browsing by Author "Mramba, Peter Thobias"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Ruwaza za toni katika vitenzi na nomino za kirombo(University of Dar es Salaam, 2020) Mramba, Peter ThobiasUtafiti huu unahususu Ruwaza za Toni katika Vitenzi na Nomino za Kirombo. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza ruwaza za ujitokezaji wa toni katika vitenzi na nomino za Kirombo na kanuni zinazotawala utokeaji huo. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru kwa kutumia Mkabala wa Tonijuu Msingi kama ulivyoasisiwa na Goldsmith (1976) na kuboreshwa na wanazuoni mbalimbali katika taaluma ya tonolojia. Utafiti ulifanyikia katika Vijiji vya Mengwe Juu na Mengwe Chini, Kata ya Mengwe, Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Wango la utafiti ni nomino na vitenzi na wazungumzaji wazawa wa Kirombo. Aidha, mbinu ya usampulishaji iliyotumika ni Nasibu Tabakishi. Pia, Mbinu za ukusanyaji data zilizotumika ni: mahojiano na ushuhudiaji. Katika mahojiano nomino na vitenzi viliandaliwa kwa Kiswahili na watoataarifa walihitajika kuyatamka kwa Kirombo huku mtafiti akirekodi na kualamisha toni katika maneno hayo. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna ruwaza mbalimbali za kitoni zinazoleteleza utokeaji wa kanuni za kitoni ambazo hutofautiana kutegemeana na idadi ya silabi na uwepo au kutowepo kwa yambwa. Kwa vitenzi na nomino za silabi moja hutawaliwa na kanuni ya uhusishaji wa tonichini na vitamkwa na sharti la ukubalifu, wakati vitenzi na nomino za silabi tatu hadi ama tano au sita za shina hutawaliwa na kanuni ya msambao wa tonijuu kuelekea kulia mwa shina, uhamaji wa TJM kutoka silabi ya kwanza kwenda katika silabi ya pili ya shina, unakiliji wa TJM katika silabi ya mwisho kasoro moja. TJM katika vitenzi na nomino za silabi moja ya shina hubiruka nyuma na khupachikwa katika kiambishi awali kwa nomino na vitenzi visoukomo sahili, wakati TJM hupachikwa katika mofimu ya yambwa kwa vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja ya shina. Pia, kwa upande wa vitenzi visoukomo sahili matokeo yanaonesha kwamba kuna TJM mbili, yaani, ya kwanza ni ya yambwa na ya pili ikiwa ya shina, ambapo katika mchakato wa ukokotozi wa uibuzi wa toni, TJM ya shina hudondoshwa kwa kuwa yambwa ina nguvu zaidi. Aidha, inapendekezwa tafiti fuatizi zifanyike katika viwango vya kirai na sentensi, uradidi katika nomino na vitenzi na tonolojia linganishi katika jamiilugha za Kichaga. Utafiti huu umesaidia kujua namna toni zinavyojitokeza katika Kirombo kwa ujumla.Item Uchunguzi wa athari za Kirombo katika jifunzaji wa kiswahili Vipengele vya kifonolojia na kimofolojia(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 2015) Mramba, Peter ThobiasSuala la athari za L1 katika ujifunzaji wa Kiswahili kama L2 limewavuta wataalamu wengi. Hata hivyo, hakuna utafiti ambao umefanyika katika lugha ya Kirombo. Kwa hiyo utafiti huu ulichunguza athari za Kirombo katika ujifunzaji wa Kiswahili kama L2 kwa kubainisha athari, sababu za athari hizo na njia za kukabilia na athari hizo. Aidha, utafiti umefanyika katika kata za Mengwe Juu, Mengwe Chini, Manda Juu, Mamsera Juu, Mamsera Chini na Manda Chini, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Ili kufanikisha kazi hii, Nadharia ya Mwingiliano Lugha iliongoza utafiti huu, yaani ujipatajiwa L2 utawezekanaikiwanaikiwatumjifunzajianamwingilianowakaribunalughainayojifunzwa. Mbinu za utafiti zilihusu: usampulishaji, ukusanyaji, uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Data ya utafiti ni ya kutoka uwandani ambapo athari zilichambuliwa na kuwekwa katika makundi mawili; athari za kifonolojia na za kimofolojia kundi. Kazi imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza, imeeleza kiini cha utafiti na utaratibu uliozingatiwa katika kufanikisha utafiti. Sura ya pili, imeshughulikia mapitio ya maandiko kuhusiana na athari za L1 katika ujifunzaji wa L2. Mapitio haya yamebainisha kuwa athari za L1 katika ujifunzaji wa L2 zipo. Sura ya tatu, imehusu mbinu za utafiti ambapo populesheni, sampuli, usampulishaji pamoja na njia tatu za ukusanyaji data zilibainishwa. Sura ya nne, imeshughulikia uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Kwa ujumla data, iliyopatikana imechanganuliwa kwa njia ya maelezo na kanuni. Nadharia ya Mwingiliano Lugha ya Schuman (1978) ndiyo iliyoongoza mjadala na uchanganuzi wa data hii. Sura ya tano imeshughulikia matokeo, hitimisho, na tafiti fuatishi. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwepo kwa athari za kimatamshi 13 ambapo baadhi hutokana na kukosekana kwa sauti katika mfumo wa sauti za lugha ya Kirombo, na vighahiri. Pia, yamebainisha athari zinazotokana na utohoaji wa msamiati, na utofauti wa maumbo ya umoja na wingi ya ngeli kati ya Kirombo na Kiswahili, ambapo huleteleza athari za L1katika ujifunzaji wa L2 kama nadharia yetu invyodai kuwa, athariza L1 za kimatamshi, kitahajia, kisarufi na kimsamiati hujitokeza katika L2 wakati wa ujifunzaji. Pia, katika kufanya jitihada za matamshi ya L2, mwanafunzi huathiriwa na sauti zilizomo L1.