Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Author "Asajile, Tusekelege"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Mchango wa msamiati wa jamiilugha za wavuvi katika Kiswahili: Mafia na Ilemela(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 2012) Asajile, TusekelegeUtafiti huu unachunguza na kubainisha Mchango wa Msamiati wa Jamiilugha ya Wavuvi katika Kiswahili hususan Kilindoni - Mafia na Mwaloni - Ilemela. Utafiti upo katika mlengo wa taaluma ya Isimujamii kwa kuwa utajihusisha na misamiati ya Jamiilugha ya wavuvi jinsi inavyotumiwa katika Jamiilugha hizo. Pili misamiati hiyo itahusianishwa na maana zilizopo katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Utafiti umefanyika katika maeneo mawili tofauti ya uvuvi, eneo zinapofanyika shughuli za uvuvi na maeneo waishio jamiilugha ya wavuvi kwa kiasi kidogo. Hii itasaidia kuona kwa namna gani misamiati hiyo inavyoweza kutumiwa na jamiilugha za wavuvi. Ni matarajio yetu kuwa utafiti utachangia kwa kiasi kikubwa katika msamiati wa Kiswahili. Zaidi ya watafitiwa 50 wametafitiwa ana kwa ana mmoja mmoja na pia kwa njia ya mahojiano katika vikundi. Uteuzi wa watafitiwa umefanywa kiholela ili kutoa fursa sawa kwa rika na jinsia tofauti. Utafiti huu umetumia vidadisi, mahojiano na kusikiliza mazungumzo ya wanajamiilugha ya wavuvi na kuyarekodi kimaandishi. Tafiti nyingi zilizofanywa zilijikita katika kuchunguza msamiati katika lugha kwa ujumla na kuangalia sababu mbalimbali za mabadiliko ya maana za misamiati na si katika kuangalia lugha jinsi inavyotumika katika jamiilugha mahsusi. Utafiti huu umekusanya na kuchanganua misamiati ya jamiilugha ya wavuvi wa eneo la Mwaloni (Ilemela) na Kilindoni (Mafia) na jinsi wanavyoitumia misamiati hiyo kama matokeo ya utafiti yalivyojiibua kutokana na uchambuzi wa data.