Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Author "Ally, Rehema Bakari"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Jinsi kitenzi kinavyojithihirisha katika kiswahili(University of Dar es Salaam,, 2012) Ally, Rehema BakariTasinifu hii ni zao la utafiti ulioshughulikia Jinsi Kitenzi ‘kuwa’ Kinavyojidhihirisha katika Kiswahili Kimsingi ripoti hii ya utafiti imcgawanyika katika sura kuu tano. Sura ya kwanza imcshugulikia utangulizi. Kwa ujumla imcangalia kwa upana historia ya lugha ya Kiswahili, tatizo la utafiti na kiunzi cha Nadharia. Sura ya pili imcangazia mapitio mbalimbali ya maandishi na tafiti zilizotangulia zinazohusiana na mada. Sura ya tatu imetalii mbinu anuai zilizotumika kufanya utafiti huu. Sura ya nne imejikita zaidi katika uchanganuzi wa data ulioibua mchango na mawazo mapya ya utafiti huu na sura ya mwisho imetumika kutoa muhtasari na hitimisho la tasinifu nzima. Kwa ujumla matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa kitenzi 4kuwa' kinajidhihirisha katika maumbo mbalimbali ambayo huwa na dhima tofauti kulingana na matumizi yake katika lugha ya Kiswahili. Maumbo hayo hubadilika kulingana na wakati na hali mbalimbali ambazo wasemaji wa lugha ya Kiswahili wamejiundia ili kukamilisha haja yao kuu ya mawasiliano. Kiumbo mabadiliko yanajidhihirisha katika wakati uliopo ambapo umbo ‘ni’/‘si’ hutumika kwa nafsi zote tofauti na ilivyo katika vitenzi vingine. Halikadhalika katika wakati uliopo yapo maumbo kama‘yu YtuYm(mu)’ n.k ambayo hutumika hasa katika lahaja za Pwani. Sanjari na hayo, utafiti huu umebaini kuwa kitenzi ‘kuwa’ chaweza kutumika kama kitenzi kikuu (kishirikishi) au kisaidizi kulingana na dhima inachobebeshwa katika tungo. Pia tumeona kuwa vijalizo vyake mara nyingi vyaweza kuwa nomino, kivumishi au wakati mwingine kirai kihusishi. Vilevile hutumika kama kibainishi katika baadhi ya tungo za Kiswahili. Wakati mwingine hujidhihirisha katika hali ya ukapa kwa kutumia umbo sauti. Kwa ujumla utafiti huu umeabaini kuwa kitenzi hiki hujibainisha katika maumbo tofauti tofauti tena wakati mwingine ubadilikaji wake haufuati kanuni au ruwaza zinazoelezeka au kutabirika kwa urahisi.