Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Author "Ally, Laila"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Athari ya utendaji simulizi katika mabadiliko ya ushairi andishi wa kiswahili uchunguzi wa diwani za e. Kezilahabi - dhifa na karibu ndani(University of Dar es Salaam, 2015) Ally, LailaUtafiti huu umechunguza athari ya utendaji simulizi katika mabadiliko ya ushairi andishi wa Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka diwani za E. Kezilahabi za Dhifa (2008) na Karibu Ndani (1988). Aidha, ili kuweza kuona namna mabadiliko na miundo mipya ya ushairi wa Kiswahili ilivyozuka, matumizi ya mbinu za fasihi simulizi, ambazo zo katika utafiti huu tumeziita vipengele vya utendaji simulizi yamechunguzwa. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za maktabani pamoja na uwandani. Mbinu za maktabani zilihusisha usomaji wa diwani mbili za Kezilahabi, Dhifa na Karibu Ndani kwa lengo la kubaini mbinu mbalimbali za utendaji simulizi alizotumia mtunzi katika mashairi yake. Kwa upande mwingine, mtafiti alitumia mbinu za utafiti wa uwandani kwa kuwahoji wadau mbalimbali wa taaluma ya ushairi wa Kiswahili kuhusiana na ujitokezaji wa vipengele vya utendaji simulizi katika Dhifa na Karibu Ndani, dhima za vipengele hivyo pamoja na athari zake katika mabadiliko ya ushairi andishi wa Kiswahili. Uchambuzi wa data za utafiti huu ulifanyika kwa kutumia misingi ya nadharia ya naratolojia pamoja na nadharia ya fomula simulizi. Misingi ya nadharia ya naratolojia iliyotumika katika utafiti huu imedondolewa kutoka katika kiunzi cha nadharia ya naratolojia kama kilivyoasisiwa na kuendelezwa na Bal (1997), Genette (1988) na Monika (2009). Nadharia hii imesaidia kujadili masuala yanayohusiana na matumizi ya vipengele vya utendaji simulizi. Masuala hayo ni pamoja na usimulizi, nafsi za usimulizi na njeo za usimulizi. Kwa upande mwingine, mjadala wa athari ya utendaji simulizi katika mabadiliko ya ushairi andishi wa Kiswahili uliongozwa na nadharia ya fomula simulizi kama ilivyoelezwa na Parry (1971) na Lord (1981). Kutokana na uchunguzi uliofanyika katika utafiti huu imedhihirika kuwa diwani za Karibu Ndani na Dhifa zimesheheni matumizi ya mbinu mbalimbali za utendaji simulizi. Mbinu hizo ni pamoja na matumizi ya visasili, mbinu za usimuliaji, ujazilizaji wa usimulizi katika wakati uliopo, ujao na uliopita, matumizi ya miundo ya fasihi simulizi, taswira, matumizi ya tashibiha, matumizi ya mbinu ya ukiushi pamoja na takriri. Vilevile mtokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa matumizi ya vipengele vya utendaji simulizi yameathiri ushairi andishi wa Kiswahili kifani na kimaudhui. Kusheheni kwa vipengele vya utendaji simulizi katika ushairi andishi wa Kiswahili - Dhifa na Karibu Ndani kunaimarisha hoja zinazoshadidia kuwa ushairi wa Kiswahili umetokana na fasihi simulizi ya Kiafrika.