Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Author "Ali, Saumu Iddi"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Athari za mtindo katika kuibua maudhui: mifano kutoka bembelezi za Pemba(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 2013) Ali, Saumu IddiUtafiti huu unachunguza namna mtindo unavyoibua maudhui kwa kutumia mifano kutoka bembelezi za Pemba. Baada ya kuona kuwa wataalamu wengi wamesema bembelezi humhusu mama na malalamiko yake tu na wala hazimuhusu mtoto anayeimbiwa. Kutokana na maudhui mazito yanayojitokeza katika nyimbo hizo kama vile ndoa ukewenza, mapenzi na kadhalika. Utafiti huu ulilenga kubaini ni mbinu zipi zitumikazo kusawiriwa maudhui hayo na wakati huo huo mtoto akafarijika akanyamaza na akapata usingizi. Mbinu zitumikazo kama vile sauti ya upole, yenye kusihi na viitikio vyake ambavyo hurudiwarudiwa kwa mahadhi ndio humlaghai mtoto akanyamaza kulia na hata akajisikia kulala. Ili kufanikisha hayo mtafiti alitumia mbinu ya kupitia machapisho mbalimbali na kwenda uwandani kupata nyimbo, vyanzo vya nyimbo na maana zake. Baada ya kupata data mtafiti alichanganua na kufanya mjadala kwa kuhusisha na nadharia ya Uchambuzi wa Matini na Mwingiliano Matini. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa bembelezi asili yake haikuwa na makusudi hayo bali kina mama walizipata kutoka katika ngoma mbalimbali na walikuja kuzitumia katika matumizi yao yakiwamo haya ya kubembelezea watoto ambapo ziliongezwa, kupunguzwa na hata kubadilika kulingana na tukio, eneo na mambo yaliyozuka katika jamii. Baada ya kuhakiki sampuli ya nyimbo imebainika kuwa bembelezi husawiri kina mama, baba na watoto pia, sio kama ilivyozoeleka ni kwa ajili ya kina mama tu kutoa dukuduku lao au kwa ajili ya watoto tu ili walale au wanyamaze kulia. Ingawa hizo baadhi zinazowahusu watoto sio katika umri huo walio nao bali mpaka wakuwe wakubwa. Ingawa utafiti huu umechunguza kipengele cha mtindo katika kuibua maudhui na hadhira lengwa bado kuna maeneo yanahitaji utafiti wa kina. Maeneo hayo ni ishara na picha, falsafa katika bembelezi na fasihi simulizi kwa ujumla wake katika kisiwa cha Pemba.