Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Author "Abdul, Atiba"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Maana na sababu za kiisimujamii kwenye majina ya koo za Kiluguru(The university of Dar es Salaam, 2013) Abdul, AtibaUtafiti huu ulihusu majina ya koo za jamii ya Waluguru ambao wanapatikana upande wa Mashariki mwa nchi ya Tanzania. Utafiti ulifanyika katika Wilaya ya Morogoro Vijijini kwa kuhusisha vijiji vitano ambavyo ni Rudewa, Kinole, Tegetero, Mkuyuni na Mifulu. Jumla ya watafitiwa arobaini walihusika katika kutoa taarifa zilizohusiana na mada ya utafiti . Watafitiwa hao waliteuliwa kwa kutumia njia mbili ambazo ni njia ya usampulishaji nasibu na njia ya usampulishaji tajwa. Kadhalika data ilikusanywa kutoka kwa watafitiwa kwa kutumia njia tatu ambazo ni njia ya usaili/ mahojiano, njia ya hojaji na njia ya ushiriki. Malengo ya utafiti huu yalikuwa mawili nayo ni kubaini Maana za Majina ya Koo za Kiluguru na kubaini Sababu za Kiisimujamii kwenye Majina ya Koo za Kiluguru. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni ya Makutano na Mwachano ya Giles ya mwaka 1982. Nadharia hii ilitumika ili kuonesha jinsi majina ya koo katika jamii ya Waluguru yanavyowiana na kutofautiana hususani katika kipengele cha maana na sababu za kiisimujamii kwenye majina ya koo hizo. Utafiti huu ulibaini kwamba, maana na sababu za kiisimujamii kwenye majina ya koo za Kiluguru huukiliwa na mambo mbalimbli yakiwemo majina ya wanyama, majina ya mimea,matukio yaliyojitokeza katika jamii, hali tabia za watu, mwonekano wa watu, majina ya makazi, ujuzi/shughuli za watu, majina ya vitu na majina ya makabila mengine. Pia utafiti ulibaini kwamba baadhi ya majina maana zake huwa katika mahusiano yaani uwepo wa jina moja hupelekea kuwepo kwa majina mengine. Vilevile utafiti ulibaini kwamba baadhi ya majina yalikuwa yakibadilika kutokana na matukio yaliyojitokeza katika koo husika na umbali wa kijiografia. Halikadhalika utafiti ulibaini kwamba majina ya koo katika jamii ya Waluguru yalikuwa yakitolewa kwa kuzingatia jinsi za wahusika. Mwisho utafiti ulibaini kwamba majina ya koo katika jamii ya Waluguru yapo katika kategoria nne za maneno ambazo ni nomino, vitenzi, vivumishi na vielezi.