Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Author "Abdalah, Fatuma"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Uingizaji wa semi katika kamusi ya kiswahili sanifu (2013) Mifano kutoka katika Methali, Nahau na Misemo(University of Dar es Salaam, 2014) Abdalah, FatumaUtafiti huu ulikusudia kuchunguza uingizaji wa semi katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Tatu la mwaka 2013. Lengo likiwa kubaini namna semi zilivyoingizwa, kubainisha upungufu uliojitokeza na kupendekeza mbinu za kukabiliana na upungufu huo. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani na uwandani. Katika utafiti wa maktabani Toleo la Tatu la Kamusi ya Kiswahili Sanifu lilichunguzwa ili kubaini namna semi zilivyoingizwa. Utafiti wa maktabani pia ulijikita katika kuchunguza kazi za watafiti mbalimbali waliomakinikia Kamusi ya Kiswahili Sanifu ingawa kazi zao zilijikita katika matoleo ya nyuma ya kamusi hii. Katika utafiti wa uwandani mbinu za hojaji na usaili zilitumika wakati wa kukusanya data za utafiti huu. Data zilizopatikana zilichambuliwa kwa kutumia njia ya maelezo na njia ya kitakwimu. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Maana ni Matumizi iliyoasisiwa miaka ya 1930 na Wittgenstein na kuiendeleza zaidi katika taaluma ya isimu mwaka (1953). Nadharia hii inasisitiza kueleza maana kwa kuzingatia matumizi ya maneno. Nadharia ya Maana ni Matumizi ilichaguliwa kuchambulia semi kwa kuwa inazingatia muktadha wa matumizi wa neno linalohusika katika kueleza maana. Hii ni kwa sababu maana ya semi haipatikani kwa kuangalia neno mojamoja linalounda semi hiyo bali huzingatia muktadha wa matumizi ya neno hilo na uhusiano kati ya neno moja na jingine. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba ingawa semi ni kipengele muhimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu, kipengele hiki hakijafanyiwa kazi ipasavyo na hivyo kinakabiliwa na upungufu mkubwa. Miongoni mwa upungufu unaokikabili kipengele cha uingizaji wa semi katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu ni kukosekana kwa kanuni maalumu ya kuingiza semi na semi nyingi kutofafanuliwa wala kutolewa maelezo ya kina. Katika utafiti huu inapendekezwa kwamba kuna umuhimu wa kuwa na kanuni maalumu ya kuingiza semi katika kamusi na kwamba semi zote zilizoingizwa katika kamusi ni vema zikafafanuliwa ili kuwasaidia watumiaji wa kamusi kuzielewa vema.