Athari za kiutamaduni katika tafsiri mifano kutoka matini za Kitalii katika makumbusho za Tanzania
dc.contributor.author | Jilala, Hadija | |
dc.date.accessioned | 2019-10-31T07:08:07Z | |
dc.date.accessioned | 2020-01-07T16:26:50Z | |
dc.date.available | 2019-10-31T07:08:07Z | |
dc.date.available | 2020-01-07T16:26:50Z | |
dc.date.issued | 2014 | |
dc.description | Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8702.J54) | en_US |
dc.description.abstract | Utafiti huu umeshughulikia athari za kiutamaduni zijibainishazo katika tafsiri kwa kuchambua matini za kitalii zilizopo katika Makumbusho za Tanzania. Nia ya kufanya hivyo ni kuibua modeli ya kutafsiri matini za kiutamaduni ambayo itakuwa kiunzi cha kutafsiri matini za kiutamaduni ili kudhibiti mapungufu ya kimawasiliano. Dira iliyoongoza katika utengenezaji wa modeli ni matokeo ya utafiti huu na mhimili wa mawazo ya Nadharia ya Skopos. Ili kuibua Modeli ya Mawasiliano ya Kiutamaduni, tulitathmini mbinu za kutafsiri matini za kiutamaduni, mikakati iliyotumika katika uteuzi wa visawe vya kiutamaduni, mapungufu ya kimawasiliano yanayosababishwa na athari za kiutamaduni na namna tunavyoweza kukabiliana nayo. Data za utafiti huu zilipatikana kwa kutumia mbinu za usomaji wa machapisho, dodoso, usaili, uchunguzi shirikishi na upimaji. Utafiti huu umegundua kuwa, mbinu zinazotumika kutafsiri matini za kiutamaduni hazina uangavu na hivyo kusababisha mapungufu mengi ya kimawasiliano. Kichochezi kikuu cha mapungufu ya kimawasiliano ni mwachano wa kiutamaduni baina ya utamaduni chanzi na utamaduni lengwa. Ili kupunguza dosari hizo, utafiti huu umependekeza Modeli ya Mawasiliano ya Kiutamaduni (MMK) ambayo ni kiunzi cha kutafsiri matini za kiutamaduni ili kuleta ufanisi wa mawasiliano. Mhimili mkuu wa modeli hii ni fikra kwamba, ujumbe wa matini ya kiutamaduni ndiyo huukilia mbinu za tafsiri. Aidha, utafiti huu umebaini kuwa mbinu inayofaa kutafsiri matini za kiutamaduni ni “uasilishaji na ufafanuzi wa visawe”. Mbinu hii ndiyo nguzo kuu ya Modeli ya Mawasiliano ya Kiutamaduni. | en_US |
dc.identifier.citation | Jilala, H. (2014) Athari za kiutamaduni katika tafsiri mifano kutoka matini za Kitalii katika makumbusho za Tanzania, Doctoral dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam | en_US |
dc.identifier.uri | http://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3539 | |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | University of Dar es Salaam | en_US |
dc.subject | Swahili language | en_US |
dc.subject | Translating into English | en_US |
dc.subject | English language | en_US |
dc.subject | Tanzania | en_US |
dc.title | Athari za kiutamaduni katika tafsiri mifano kutoka matini za Kitalii katika makumbusho za Tanzania | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |