Fomula simulizi katika tenzi andishi za Kiswahili : mifano kutoka utenzi wa rasi' Lghuli na utenzi wa vita vya wadachi kutamalaki Mrima
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umejadili Fomula Simulizi katika Tendi Andishi za Kiswahili kwa kutumia mifano kutoka Utenzi wa Rasi '1Ghuli na Utenzi wa Vita vya Wadachi Kutamalaki Mrima. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani, ambapo matini nyingi zilisomwa ili kupata ruwaza ya jumla kuhusu Fomula Simulizi katika tendi andishi za Kiswahili. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Fomula Simulizi. Nadharia hii iliibuka kutokana na tatizo la Homer kati ya karne ya 19 na 20. Aidha waasisi wa nadharia hii wanadai kwamba, mtendaji wa tendi simulizi mrefu huweza kutunga utungo mrefu papo kwa papo kwa kutumia Fomula Simulizi. Utafiti umebaini kuwa sifa za fomula simulizi katika tench andishi za Kiswahili ni kuwa hutosheleza kigezo cha urefu, vina na mizani na hufanya utunzi kusadifu usimulizi. Pia umegundua utokeaji wa vipengele mbalimbali vya fomula simulizi katika tenth andishi za Kiswahili kama vile topo, uradidi na unyambulishaji. Aidha dhima ya fomula simulizi katika tendi andishi za Kiswahili zimebainishwa.Utafiti umehitimisha kwamba, utokeaji wa Fomula Simulizi katika Tendi andishi za Kiswahili na tendi simulizi unafanana kwa kiasi kikubwa sana ingawa kipengele kinachotawala zaidi katika tendi andishi za Kiswahili ni topo. Ingawa utunzi wa tendi andishi na simulizi ni tofauti sana, matumizi ya fomula Simulizi katika tendi andishi za Kiswahili hayawezi kukwepeka kwani tendi zote zinahusika na usimulizi. Tunapendekeza kuwa uchambuzi wa tendi simulizi usitofautishwe sana na uchambuzi wa tendi andishi ingawa utunzi wa tendi hizo ni tofauti kabisa. Tunasema hivyo kwa sababu utafiti huu imebainika kuwa vipengele vya fomula simulizi vilivyojitokeza katika tendi andishi ndivyo hujitokeza katika tendi simulizi. Pia sifa na dhima ya matumizi ya fomula simulizi katika tenth andishi zinawiana kwa kiasi kikubwa na za tendi simulizi.