Dhima ya mwanamke katika kuibua dhamira za nyimbo za sherehe za mwaka kogwa katika jamii ya Makunduchi

Date

2019

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Chuo kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Tasnifu hii imejikita kujadili dhima ya mwanamke katika kuibua dhamira za nyimbo za sherehe za mwaka Kogwa katika jamii ya Makunduchi Zanzibar. Tasnifu imejngeka kuptia malengo mahsusi matatu. Lengo la kwanza lilikuwa ni kubainisha dhima ya mwanamke katika nyimbo za sherehe za mwaka Kogwa katika jamii ya kimakundchi. Lengo la poli lilihusu kueleza dhamiara zinazoibuliwa kupitia dhima ya mwanamke sherehe za mwaka Kogwa. Lengo la tatu lililenga kufanunua sababu za mwanamke kubeba dhima katika nyimbo za sherehe Kogwa katika jamii ya kimakundchi. Data za utafiti huu zimekusanywa kutoka maktabani na uwandani. Mbinu kadhaa zilitumika katika kukusanya data hizo kama vile udurusu wa Makunduchi. Nadharia ya Ufeministi wa kiafrika pamoja na ile ya Uhalisia ndizo zilizotuongoza katika uchambuzi wa data za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa mwanamke katika nyimbo za sherehe za mwaka Kogwa katika jamii ya kimakunduchi amebeba dhima kadhaa kama vile kuimba nyimbo za kukamilisha sherehe, kupika vyakula vya sherehe, na kuonesha usawiri wa mwanamke katika nyimbo hizo. Usawiri huo ni pamoja na mwanamke ni mpangaji masharti ya tendo la ndoa, mwanamke ni mzazi na mlezi wa familia, mwanamke ni mwanamapinduzi na mwanamke ni kiumbe anayenyanyaswa. Dhamira zinazoibuliwa kuptia dhima ya mwanamke katika nyimbo za mwaka Kogwa ni uhifadhi wa utamaduni wa jamii, upishi wa vyakula, ueneaji wa UKIMWI, malezi kwa wanajamii, mapenzi na ndoa, na utetezi wa mwanamke. Aidha, utafiti umebaini sababu kadhaa za mwanamke kubeba dhima katika nyimbo za sherehe za mwaka Kogwa za jamii ya Makunduchi. Sababu hizo ni pamoja na nafasi ya mwanamke katiaka jamii, uzalendo wa mwanamke katiaka kuendeleza utamaduni wa jamii, kutimiza baadhi ya mahitaji, umuhimu wa mwanamke katika malezi ya jamii, na mahitaji ya mabadiliko katiaka jamii. Utafiti pia umetoa mapendekezo kadha wa kadha kwa tafiti zijazo.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF ML3849.T34K42)

Keywords

Music and literature, Music, Music theater, Tanzania

Citation

Rajab , J K ( 2019) Dhima ya mwanamke katika kuibua dhamira za nyimbo za sherehe za mwaka kogwa katika jamii ya Makunduchi, Master dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.