Ufasihi simulizi katika riwaya ya kisasa ya Kiswahili: mifano kutoka Nagona (1990) na Mzingile (1991)

Date

2012

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kubainisha namna ufasihi simulizi unavyojitokeza katika riwaya teule za Kezilahabi Nagona (1990) na Mzingile (1991). Lengo hili limeweza kufanikiwa kutokana na kukamilika kwa malengo mahususi yaliyohusu kubainisha utokezaji wa ufasihi simulizi katika riwaya teule, na kueleza dhamira mbalimbali zilizotuwezesha kupata na kuchopoa ufasihi simulizi katika riwaya teule. Kazi hii na malengo kusudiwa katika muktadha wa kumtathimini Kezilahabi kifani na kimaudhui kupitia riwaya teule kulikuwa kugumu, ila kumekamilika kitaaluma. Maandiko na machapisho mbalimbali yanayohusiana na mada ya utafiti ambayo yamepitiwa kwa kina kwa kuongozwa na nadharia ya Simiotiki, yameshadidia kukomaa kwa kazi husika. kwa upande wa uchambuaji, uchakataji na usanifishaji wa data, utafiti umetumia mbinu ya uchambuzi wa kimaudhui. Hiki ndicho kinachotumakinisha kwenye uchambuzi wa data kuwa, umefanywa kwa kuongozwa na mbinu ya uchambuzi wa kimaelezo ya kifasihi sambamba na mkabala wa kidhamira. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa Kezilahabi anatumia sana vipengele vingi vya kifasihi simulizi katika riwaya zake hususani teule tulizozichambua. Baadhi ya vipengele hivyo ni wahusika wa kifasihi simulizi, mandhari, utamaduni mila na desturi, nafasi ya mwanamke katika jamii, mwanamke na suala la haki, matumizi ya taswira na ishara, matumizi ya mafumbo, tanakali sauti, mwingiliano wa tanzu, ucheshi na dhana ya ukimya. Baada ya kutathmini juu ya mwandishi Kezilahabi kifani na kimaudhui, tumebaini kwamba ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Ukweli huu ulianza kwa kuihakiki vilivyo hoja ya Mbatiah (1998) na kuonesha kwamba, kazi za Nagona (1990) na Mzingile (1991) ni riwaya muhimu katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili na zimeleta mabadiliko makubwa katika muundo, mtindo, wahusika, matumizi ya lugha, mandhari ya kidhanaishi na mabadiliko katika uelezaji wa maudhui.Mwisho, tumetoa hitimisho kuu la utafiti ambalo kwalo tumeainisha maeneo mbalimbali ya kiutafiti yanayoweza kuibuliwa katika riwaya teule na riwaya ya kisasa ya Kiswahili kwa ujumla.

Description

Keywords

Swahili literature, Nagona (1990), Mzingile (1991)

Citation

Lindi, L. M (2012) Ufasihi simulizi katika riwaya ya kisasa ya Kiswahili: mifano kutoka Nagona (1990) na Mzingile (1991), Tasinifu ya M.A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)