Kiburi kinavyoficha unyonge: mifano kutoka riwaya za C.S.L Chachage
No Thumbnail Available
Date
2006
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Kiburi hujitokeza kwa ajili ya unyonge . hili ni dai la mwanasaikolojia A. aldler. Kutokana na wazo lake, ni kwamba kila mtu akiwa na hisia ya unyonge, anajaribu kupambana na kuishinda hali hiyo. Lakini hisia ya unyonge ikiwa kubwa, mwenye unyonge anatafuta jinsi ya kuuficha unyonge wake na kuonesha ubora zaidi kutokana na hofu ya kushindwa na hisia hiyo. Hivyo ndivyo kiburi kinavyojijenga ndani ya mtu. Katika riwaya ya Chachage, tunaona wahusika wenye kiburi kutokana na elimu zao, utajiri wao, madaraka yao, na kadhalika. Tasnifu hii inaangalia jisni hawa ahusika wanavyotumia kiburi kwa kuuficha unyonge wao, ambao unatokea kutokana na malezi yasiyofaa, aumatatizo kwenye uhusiano katika familia au jamii. Hali kadhalika, Adler anaeleza kwamba wenye kiburi wanaangalia manufaa yao wenyewe tu bila kuwajali watu wengine. Lakini anadai kwamba watu hao wakiguswa na hisia za watu wengine au hisia za jamii, wanaweza kubadilika. Tasnifu hii inachunguza mabadiliko ya wahusika wenye kiburi yanasawiria vipi katika riwaya za chachage. Kwa kufanya hivyo, tunaelewa zaidi dhima ya kiburi, umuhimu wa uhusiano mzuri katika kukipiga vita kiburi katika jamii, na mchango wa riwaya za Chachage katika jam
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.A32)
Keywords
Swahili literature, Folk literature, Swahili language
Citation
Adachi, F (2006) Kiburi kinavyoficha unyonge: mifano kutoka riwaya za C.S.L Chachage.Master dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.