Dhima ya visasili katika jamii ya Wagogo.

dc.contributor.authorMbijima, Rose Jackson
dc.date.accessioned2020-02-18T14:09:51Z
dc.date.available2020-02-18T14:09:51Z
dc.date.issued2011
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8208.M3254)en_US
dc.description.abstractVisasili ni utanzu mmojawapo wa fasihi simulizi unaopatikana katika jamii nyingi za Afrika na ulimwcngu kwa ujumla Visasili ni hadithi za kale zenye kuwakilisha imani na mtazamo wa jamii inayohusika kuhusu asili ya ulimwengu na mwenendo wake, kuhusu asili yao wenyewe na namna na shabaha ya maisha yao. Utafiti huu unahusu uchunguzi wa visasili katika jamii ya Wagogo. Utafiti ulikuwa na malengo mawili, kubainisha visasili vya Kigogo na kuhakiki dhima ya visasili hivyo Katika kufanikisha malengo ya utafiti, nadharia ya kiuamilifu imetumika katika uchanganuzi wa data. Data ilikusanywa kutoka mkoa wa Dodoma. Mbinu ya mahojiano ilitumika katika zoezi la kukusanya data sambamba na matumizi ya hojaji na kanda zilizorekodiwa na walaalamu wengine kuhusu visasili na zile alizorekodi mtafiti wakati akiwa uwandani. Utaflti ulibaini visasili viwili katika jamii ya Wagogo, ambavyo ni kisasili cha "Wang'omvya rafiki wa simba" na kingine ni "Babu asiyekuwa na shukrani." Dhima za visasili zilizobainishwa kwa kuzingatia visasili viwili vilivyopatikana katika utafiti. Kama tanzu nyingine za fasihi simulizi, utanzu wa visasili una mchango mkubwa katika maisha ya kila siku ya mwana jamii. Huelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali hasa yale yaliyotokea zamani na yanayoaminika kuwa ni ya kweli na yanaeleza kuhusu asili ya mambo kadha wa kadha katika jamii Visasili huonesha utamaduni wa jamii husika hasa kupitia kwenye ibada za miviga na matambiko. Ni utanzu unaoturudisha nyuma kabisa kuona historia ya Mwafrika kabla ya kuja kwa wageni walioleta dini mpya kutukumbusha tulikuwa tunaabudu vipi, nani, wapi na kwa namna gani Visasili ni uwanda ambao unahitaji tafiti zaidi za kitaaluma kutokana na umuhimu wake na dhima yake katikajamii. Inapendekezwa kuwa tafiti zifanywe katika vipengele vingine vya lugha, na kadhalika. Aidha, tafiti linganishi zifanywe kwa jamii tofauti tofauLi zenye visasili. Utafiti kuhusu tanzu nyingine mbali na visasili pia unaweza kufanyika katika jamii ya Wagogo, kwa mfano, hadithi za ngano methali na nyinginezo.en_US
dc.identifier.citationMbijima, R. J. (2011). Dhima ya visasili katika jamii ya Wagogo. Tasnifu ya Uzamili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/7211
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectGogo languageen_US
dc.subjectDodomaen_US
dc.titleDhima ya visasili katika jamii ya Wagogo.en_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mbijima 2011.pdf
Size:
82.69 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: