Ushujaa katika motifu ya safari ya msako: ulinganishi wa ngano za kiewe kutoka ghana na riwaya za Shaaban robert kutoka Tanzania.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2018
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu ulihusu ushujaa katika motifu ya safari ya msako ulinganishi ukiwa katika ngano za Kiewe kutoka Ghana na riwaya teule za Shaaban Robert kutoka Tanzania. Tulifanya utafiti kutokana na mgongano wa kinadharia ambapo kuna wataalamu wa fasihi wanaoona kuwa, kwa vile kila jamii ina utamaduni wake, kazi zao za fasihi hutofautiana na wengine wanaoona kuwa jamii zenye mfanano mkubwa wa kiutamaduni huweza kuwa na kazi za fasihi zinazofanana. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza na kulinganisha ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako kwenye ngano za Kiewe na riwaya teule za Shaaban Robert. Aidha, utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi manne ambayo ni: Kubainisha ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako katika ngano za Kiewe na riwaya teule za Shaaban Robert; kueleza kufanana na kutofautiana kwa ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako kwenye ngano za Kiewe na riwaya teule za Shaaban Robert; kufafanua jinsi ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako unavyobainisha utamaduni na falsafa ya Kiafrika katika ngano za Kiewe na riwaya teule za Shaaban Robert; na kubainisha dhima ya ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako kwenye ngano za Kiewe na riwaza teule za Shaaban Robert katika maendeleo ya fasihi. Ili kuweza kutimiza malengo hayo, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za aina mbili, ambazo ni majadiliano/mahojiano ya vikundi na udurusu matini. Mkabala wa uchambuzi uliotumika ni ule wa kitaamuli. Aidha, uchambuzi huo ulifanywa kwa kutumia ruwaza ya shujaa, nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika na nadharia ya Mwingilianomatini. Kuhusu matokeo ya utafiti, imebainika kuwa ngano za Kiewe na riwaya teule kwa kiasi kikubwa zimesheheni ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako. Aidha, imebainika kuwa, kuna mfanano mkubwa baina ya ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako katika ngano za Kiewe na riwaya teule. Pia, utafiti huu umebaini kuwa ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako katika tanzu husika unabainisha utamaduni na falsafa ya Kiafrika. Mwisho, utafiti huu umebainisha dhima ya ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako kwenye ngano za Kiewe na riwaza teule za Shaaban Robert katika maendeleo ya fasihi teule. Mbali na kufafanua masuala hayo, bado utafiti wa kina unahitajika katika maeneo mbalimbali. Kwanza, kuna haja ya kufanya utafiti utakaohusisha ngano nyingi zaidi na riwaya nyingine zaidi ya zilizotumika katika utafiti huu. Pia, utafiti zaidi utakaohusisha tanzu nyingi zaidi unahitajika ili kutoa mahitimisho ya kimajumui.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.S676)
Keywords
Language and languages, Swahili literature, Ngano za kiewe kutoka Ghana, Riwaya za Shaaban Robert kutoka Tanzania
Citation
Sosoo, F. K. (2018). Ushujaa katika motifu ya safari ya msako: ulinganishi wa ngano za kiewe kutoka ghana na riwaya za Shaaban Robert kutoka Tanzania. Tasnifu ya uzamivu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.
Collections