Ruwaza za uradidi wa vitenzi katika lugha ya Shisafwa

No Thumbnail Available
Date
2012
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu ruwaza za uradidi wa vitenzi katika lugha ya Shisafwa inayozungumzwa katika nyanda za juu Kusini mwa Tanzania katika wilaya za Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini na Chunya. Jumla ya kata tatu za Inyala, Tembela na Ulenje zilihusika. Utafiti huu ulichunguza ruwaza za uradidi wa vitenzi katika lugha ya Shisafwa ambapo aina za uradidi na ruwaza zake, mazingira ya utokeaji wa uradidi na dhima zake mbalimbali zilichunguzwa. Vitenzi vya namna tatu viliteuliwa: vitenzi visoukomo, vitenzi vya silabi moja na vitenzi nyambulishi. Kwa kuongozwa na Nadharia ya Uelekeani, utafiti huu ulikusudia kujibu maswali yafuatayo; kwanza, je, kuna aina ngapi za uradidi na ruwaza zake ni zipi? Pili, ni mazingira gani ambamo huukilia utokeaji wa uradidi katika lugha ya Shisafwa? Tatu, je, uradidi una dhima gani katika lugha ya Shisafwa? Utafiti huu uligawanyika katika sura tano, ambapo sura ya kwanza imeeleza taarifa za awali ikijumuisha eneo la utafiti, usuli wa utafiti, mfumo sauti wa lugha ya Shisafwa na historia ya Wasafwa. Aidha, tamko la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, na mawanda ya utafiti vilishughulikiwa katika sura hii. Sura ya pili ilihusu mapitio ya maandiko mbalimbali kuhusiana na uradidi wa vitenzi katika lugha za Kibantu na mwega wa kinadharia ulioongoza utafiti huu. Sura ya tatu ilihusu mbinu za utafiti zilizotumika katika mchakato wa kukusanya data. Hojaji, ushuhudiaji na usaili ni mbinu ambazo zilitumika kukusanyia data za utafiti huu. Aidha, sampuli ya watafitiwa 30, ambao ni wazungumzaji wazawa wa lugha ya Shisafwa ndio waliotumika katika utafiti huu. Sura ya nne ilihusu uchambuzi na uwasilishaji wa data kuhusu ruwaza za uradidi wa vitenzi katika lugha ya Shisafwa ambapo aina za uradidi wa vitenzi na ruwaza zake mbalimbali zilifafanuliwa. Pia, mazingira ya utokeaji wa uradidi pamoja na dhima zake zimechambuliwa katika sura hii. Sura ya tano ilihusu matokeo ya utafiti, hitimisho na mapendekezo.
Description
Keywords
Bantu language, Safwa language, Tanzania
Citation
Mwashota, P (2012) Ruwaza za uradidi wa vitenzi katika lugha ya Shisafwa, Tasinifu ya M.A Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)