Tathmini ya maudhui ya tafsiri katika redio ya sauti ya afrika nchini libya Mifano ya kiarabu na Kiswahili
dc.contributor.author | Elmagdouli, Sobhi | |
dc.date.accessioned | 2019-10-30T12:45:53Z | |
dc.date.accessioned | 2020-01-07T16:26:43Z | |
dc.date.available | 2019-10-30T12:45:53Z | |
dc.date.available | 2020-01-07T16:26:43Z | |
dc.date.issued | 2014 | |
dc.description | Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PJ6403.E45) | en_US |
dc.description.abstract | Utafiti huu unahusu tathmini ya maudhui ya tafsiri zinazofanywa katika Redio Sauti ya Afrika nchini Libya kutoka katika lugha ya Kiarabu kwenda Kiswahili. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kosa likifanyika katika kutafsiri matini katika vyombo vya habari, huwaathiri watu wengi kwa muda mfupi, na hivyo kupotosha jamii. Ili kutimiza lengo la utafiti huu, tulitumia mbinu tatu kukusanya data, ambazo ni mbinu ya maktabani, usaili na hojaji. Aidha, Nadharia ya Usawe wa Kipragmatiki ndiyo iliyoongoza utafiti huu na uchambuzi wa data tuliyozikusanya. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba Redio Sauti ya Afrika inatumia mchanganyiko wa istilahi; ambazo zinafanikisha uwasilishaji wa maudhui na zile ambazo zinaathiri maudhui. Kwa upande mwingine, utafiti umebaini kuwa kwa kiasi kikubwa tafsiri zilizofanywa katika Redio Sauti ya Afrika zinatumia istilahi ileile kwa wasikilizaji wa Kiswahili na hivyo kufanikisha haki ya raia kupata habari. Aidha, kuna kasoro kadhaa zilizobainika, kama zile maneno kutafsiriwa isivyo sahihi, maneno kudondoshwa na pia neno moja kutafsiriwa tofautitofauti nahivyokuathiri maudhui. Utafiti huu umebaini kuwa kasoro hizo zinatokana na mbinu ya tafsiri sisisi na neno kwa neon inayotumika na hivyo utafiti huu unapendekeza mbinu ya tafsiri ya kimawasiliano itumike katika kutafsiri matimi mbalimbali katika vyombo vya habari kwa ujumla.Utafiti huu ulijikita katika matini tu za kisiasa kwa hiyo imependekezwa pia tafiti za kina katika aina nyingine za matini, kama vile matini za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni zifanyike na kutathmini jinsi matini chanzi na matini lengwa zinavyowiana katika kuwasilisha maudhui, Aidha utafiti utakaohusisha vyombo vingine vya habari ufanywe. | en_US |
dc.identifier.citation | Elmagdouli, S. U.(2014).Tathmini ya maudhui ya tafsiri katika redio ya sauti ya afrika nchini libya Mifano ya kiarabu na Kiswahili. Master dissertation, Chuo kikuu cha Dar es Salaam. | en_US |
dc.identifier.uri | http://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3476 | |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | University of Dar es Salaam | en_US |
dc.subject | Arabic language | en_US |
dc.subject | Translating into Swahili | en_US |
dc.subject | Swahili language | en_US |
dc.title | Tathmini ya maudhui ya tafsiri katika redio ya sauti ya afrika nchini libya Mifano ya kiarabu na Kiswahili | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |