Udhaifu wa sera ya lugha ya Tanzania: nini kifanyike?
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu unaochunguza Udhaifu wa Sera Lugha Tanzania: Nini Kifanyike? ulifanyika katika mkoa wa Dar es Salaam. Utafiti huu ulihusisha jumla ya watafitiwa 30 waliotoa data kwa kutumia mbinu za mahojiano na hojaji. Utafiti huu ulitumia mkabala wa kinadharia wa Upangajilugha unaopendekezwa na Haugen (1968). Kwa kuzingatia matokeo yaliyopatikana kwa njia za hojaji na mahojiano, mtafiti amebaini udhaifu wa matamko 6 ya sera ya lugha ambayo hayajatekelezwa. Lengo lingine la utafiti huu lilitaka kujua udhaifu wa matamko ya sera ya lugha Tanzania unasababishwa na nini. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwa udhaifu wa matamko ya sera ya lugha unasababishwa na hali ya uchumi wa nchi, kasumba za viongozi wenye dhamana kutotilia mkazo masuala ya lugha, wasomi kutotoa mchango wa kuhimiza umuhimu wa lugha zetu za asili na ulegevu wa sera yenyewe kutotekelezeka. Kuhusu nini kifanyike ili kuondoa udhaifu huu wa matamko ya sera ya lugha Tanzania, watafitiwa walitoa mapendekezo yafuatayo: Kwanza, watunga sera waingize matamko muhimu ya sera ya lugha katika katiba ya nchi. Pili, viongozi wenye dhamana waelimishwe umuhimu wa lugha zetu ili zipewe hadhi zinazostahili. Tatu, sera ya lugha isiwe ndani ya sera ya utamaduni, inafaa sera ya lugha ijitegemee yenyewe. Nne, lugha ya Kiingereza na lugha zingine za kigeni zipewe nafasi ya kufundishwa vizuri ili Watanzania waweze kuwasiliana na mataifa ya nje. Mwisho, watafitiwa wanapendekeza kuwa lugha za jamii zitumike kufundishia katika miaka ya mwanzo ya elimu ili kuzilindazisipotee.