Suala la uzazi katika ontolojia ya Kibantu na jinsi lilivyojitokeza katika riwaya za kiswahili

No Thumbnail Available
Date
2012
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchambua suala la uzazi katika ontolojia ya Kibantu kama lilivyosawiriwa kwenye riwaya za Kiswahili. Utafiti ulijikita katika hoja ya kwamba suala la uzazi ni miongoni mwa maudhui nyeti ya ustaarabu wa Kibantu uliosawiriwa kwenye riwaya za Kiswahili ingawa wahakiki hawajalipa nafasi yake stahiki katika kazi zao, ama kwa kulifumbia macho kabisa au kwa kulipa nafasi ndogo sana kinyume na unyeti wake. Hivyo, kazi hii imevibainisha na kuvijadili vipengele mbalimbali vya utamaduni wa Kibantu juu ya dhana ya uzazi. Data zilizotumika katika kazi hii zimekusanywa kupitia vitabu vilivyoteuliwa na vya ziada katika riwaya za Kiswahili. Uchambuzi wa data umeongozwa na Kiunzi cha nadharia ya Ontolojia ya Kibantu na kutumia mkabala wa kidhamira. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa suala la uzazi katika ontolojia ya Kibantu lina mitazamo mikuu mitatu. Mtazamo wa kwanza, unaonyesha kuwa uzazi ni baraka na ugumba ni laana. Mtazamo wa pili ni imani kuwa uzazi ndio mhimili au nguzo ya ndoa. Na mtazamo wa tatu ni imani kuwa uzazi ndio nguzo ya ujenzi wa ukoo. Utafiti huu unaonyesha kuwa imani ya Wabantu kuhusu uzazi imejikita katika mitazamo hiyo mitatu. Hata hivyo, mtazamo mama ulioonekana kujitokeza kwa kiasi kikubwa katika riwaya takribani zote ni ule wa kuwa uzazi ni baraka na ugumba ni laana. Zaidi ya utafiti huu, hitajio bado lipo kwa tafiti nyingine kufanywa katika eneo hili kwa kuchunguza mambo kadha wa kadha katika upande huu wa ontolojia ya Kibantu. Kwa mfano, dhana ya familia pana, dhana ya ujaala, dhana ya wakati, na hadhi ya mwanamke na mwanamume katika ontolojia ya Kibantu.
Description
Keywords
Bantu language, Swahili language
Citation
Kajosi, S (2012) Suala la uzazi katika ontolojia ya Kibantu na jinsi lilivyojitokeza katika riwaya za kiswahili, Tasnifu ya M.A.Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)