usawiri wa familia pana ya kiafrika: mifano kutoka Riwaya za G. Ruhumbika na C.S. Chachage

dc.contributor.authorShaabani, Amida
dc.date.accessioned2019-07-12T10:39:31Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:38Z
dc.date.available2019-07-12T10:39:31Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:38Z
dc.date.issued2012
dc.descriptionAvailable in print formen_US
dc.description.abstractTasnifu hii inachunguza usawiri wa dhana ya familia pana katika riwaya za Kiswahili. Inalenga kuchunguza utokeaji wa dhana ya familia pana ya Kiafrika katika riwaya teule za Ruhumbika ambazo ni Miradi Bubu ya Wazalendo na Janga Sungu la Wazawa pamoja na riwaya teule ya Chachage ambayo ni Makuadi wa Soko Huria.Tasnifu imeshughulikia dhana ya familia pana ya Kiafrika kwa kubaini muundo wa familia hiyo pana, kuonesha uhusiano na majukumu ya wanafamilia na pia kubaini athari za mabadiliko ya kijamii katika familia pana.Aidha kwa kutumia nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika na Mkabala wa Kidhamira mtafiti aliweza kukusanya dhamira zinazohusiana na dhana ya familia pana ya Kiafrika katika riwaya teule na kuziorodhesha, kisha kubaini muundo wa familia pana, uhusiano na majukumu ya wanafamilia katika familia pana na athari za mabadiliko ya kijamii katika familia hiyo.Matokeo ya utafiti wa tasnifu hii yanaonesha kuwa muundo wa familia pana ya Kiafrika uliojitokeza unahusisha wazazi ambao ni baba na mama, babu na bibi, watoto tena wengi wanaozaliwa ndani ya familia pana, watoto na ndugu wengine wanaolelewa hapo, marafiki, waliokufa, watoto ambao hawajazaliwa pamoja na muundo wa familia pana katika kiwango cha jamii.Uhusiano na majukumu ya wanafamilia uliojitokeza ni pamoja na uhusiano baina ya mume na mke, uhusiano wa watoto na ndugu zao ndani ya familia, uhusiano na majukumu baina ya wazazi na watoto wao na wale wanaolelewa hapo pia uhusiano wa wanafamilia katika kiwango cha jamii. Athari za mabadiliko ya kijamii katika familia pana ni ubinafsi, usaliti, suala la utajiri, imani za ushirikina pamoja na tamaa za kimwili ambayo yanaathiri uhusiano na mshikamano wa ndugu na wanafamilia katika familia pana. Mwisho, unatolewa muhtasari wa tasnifu, hitimisho na mapendekezo.en_US
dc.identifier.citationShaabani, A(2012),usawiri wa familia pana ya kiafrika: mifano kutoka Riwaya za G. Ruhumbika na C.S. Chachage, master dissertation, University of Dar es Salaam (available at)en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3428
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectAfrican literatureen_US
dc.subjectRuhumbika,G.en_US
dc.subjectChachage,C.S.en_US
dc.titleusawiri wa familia pana ya kiafrika: mifano kutoka Riwaya za G. Ruhumbika na C.S. Chachageen_US
dc.typeThesisen_US

Files