Mchango wa msamiati wa jamiilugha za wavuvi katika Kiswahili: Mafia na Ilemela

dc.contributor.authorAsajile, Tusekelege
dc.date.accessioned2019-08-15T08:22:32Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:40Z
dc.date.available2019-08-15T08:22:32Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:40Z
dc.date.issued2012
dc.descriptionAvailable in print formen_US
dc.description.abstractUtafiti huu unachunguza na kubainisha Mchango wa Msamiati wa Jamiilugha ya Wavuvi katika Kiswahili hususan Kilindoni - Mafia na Mwaloni - Ilemela. Utafiti upo katika mlengo wa taaluma ya Isimujamii kwa kuwa utajihusisha na misamiati ya Jamiilugha ya wavuvi jinsi inavyotumiwa katika Jamiilugha hizo. Pili misamiati hiyo itahusianishwa na maana zilizopo katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Utafiti umefanyika katika maeneo mawili tofauti ya uvuvi, eneo zinapofanyika shughuli za uvuvi na maeneo waishio jamiilugha ya wavuvi kwa kiasi kidogo. Hii itasaidia kuona kwa namna gani misamiati hiyo inavyoweza kutumiwa na jamiilugha za wavuvi. Ni matarajio yetu kuwa utafiti utachangia kwa kiasi kikubwa katika msamiati wa Kiswahili. Zaidi ya watafitiwa 50 wametafitiwa ana kwa ana mmoja mmoja na pia kwa njia ya mahojiano katika vikundi. Uteuzi wa watafitiwa umefanywa kiholela ili kutoa fursa sawa kwa rika na jinsia tofauti. Utafiti huu umetumia vidadisi, mahojiano na kusikiliza mazungumzo ya wanajamiilugha ya wavuvi na kuyarekodi kimaandishi. Tafiti nyingi zilizofanywa zilijikita katika kuchunguza msamiati katika lugha kwa ujumla na kuangalia sababu mbalimbali za mabadiliko ya maana za misamiati na si katika kuangalia lugha jinsi inavyotumika katika jamiilugha mahsusi. Utafiti huu umekusanya na kuchanganua misamiati ya jamiilugha ya wavuvi wa eneo la Mwaloni (Ilemela) na Kilindoni (Mafia) na jinsi wanavyoitumia misamiati hiyo kama matokeo ya utafiti yalivyojiibua kutokana na uchambuzi wa data.en_US
dc.identifier.citationAsajile, T (2012) Mchango wa msamiati wa jamiilugha za wavuvi katika Kiswahili: Mafia na Ilemela, Tasinifu ya M. A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3453
dc.language.isoenen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectVocabularyen_US
dc.subjectMafiaen_US
dc.subjectIlemelaen_US
dc.titleMchango wa msamiati wa jamiilugha za wavuvi katika Kiswahili: Mafia na Ilemelaen_US
dc.typeThesisen_US
Files