Mabadiliko ya kijamii na riwaya ya upelelezi Tanzania

dc.contributor.authorKimura, Eiko
dc.date.accessioned2020-06-10T11:37:49Z
dc.date.available2020-06-10T11:37:49Z
dc.date.issued1991
dc.descriptionInapatikana maktaba ya Dkt Wilbert Chagula, Kitengo cha East Africana, class-mark ( THS EAF PN3448.D4K5)en_US
dc.description.abstractRiwaya ya upelelezi ni fani ya fasihi ambayo imetokea kuenea na kupendwa sana duniani. Riwaya hiyo ilianzia ulaya na marekani katika karne ya 19, na ilifika Africa katikati ya karne hii. Riwaya ya kwanza ya upelelezi katika lugha ya Kiswahili, mzimu wa watu wa kale, iliandikwa na M.s. Abdulla mwaka 1957. Tangu wakati huo, riwaya za upelelezi zimechapishwa kwa wingi Tanzania. Hasa katika miaka ya 1970-1980. Tasnifu hii inajaribu kuchambua sababu za kupendwa na kuenea kwake nchini Tanzania. Tasnifu inatetea hoja kuwa riwaya ya upelelezi inazuka wakati huu kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yaliyotokea wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni. Mabadiliko hayo ni pamoja na kupanuka kwa shughuli za kiuchumi na kijamii, hasa kuongezeka kwa viwanda na kuenea kwa elimu ya msingi nay a watu wazima, kuongezeka kwa watu,kukua kwa miji, kuenea kwa lugha ya Kiswahili na athari ya lugha na tamaduni za kigeni. Wahusika na maudhui ya riwaya za upelelezi yanaekuwa yakibadilika kufuatana na mabadiliko hayo ya kijamii riwaya za mwanzo za M.S. Abdulla zilisawiri mpelelezi binafsi aliyechunguza uhalifu uliowahusu watu wa matabaka ya juu huko Zanzibar. Riwaya za miaka ya 1960 na 1970 ziliwatumia wapelelezi wa dola (polisi na kachero) ambao walichunguza uhalifu utendekao mijini, hasa mauaji, wizi na ujambazi. Na riwaya za miaka ya 1990 zimeanza kuvuka nje ya mipaka ya Tanzania na kusimulia habari za ujasusi wa kimataifa. Kupendwa kwa riwaya hii kimsingi kulitokana na sababu au sifa za ndani za riwaya hiyo. Sifa hizo ni za kifani na za kimaudhui. Kifani, riwaya ya upelelezi inawavutia watu kwa kuwa ina athari kubwa ya fasihi simulizi (ambayo wasomaji wengi wameizoea) kimuudo na katika mbinu inazozitumia. Vilevile riwaya hiyo huvutia kutokana na taharuki, ucheshi na utamu wa lugha yake. Kimaudhui, riwaya ya upelelezi inaakisi mtazamo na mawazo ya mwanajamii wa kawaida kuhusu masuala ya uhalifu, dhuluma, urithi, tamaa, mapenzi na mapenzi haramu. Funzo lake kuwa “uhalifu haulipi” hukubalika kwa urahisi kwa wasomaji wengi, na hasa kwa watawala na viongozi wa dini. Baadhi ya riwaya zinakwenda mbele Zaidi na kutoa mawazo yahusuyo ukombozi. Kutokana na sifa hizo riwaya ya upelelezi kwa kiasi Fulani ni kioo cha jamii iliyopo, hasa ile ya mijini. Aidha ina dhima ya kufunza, kuadibu, kukuza lugha na kusahihisha jamii. Wakati huo huo, inasaidia kuburudisha watu na kuleta hali ya Amani na utangamano katika jamii.en_US
dc.identifier.citationKimura, E (1991) Mabadiliko ya kijamii na riwaya ya upelelezi Tanzania, Master dissertation, University of Dar es Salaamen_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/12297
dc.language.isootheren_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dar es Salaamen_US
dc.subjectRiwayaen_US
dc.titleMabadiliko ya kijamii na riwaya ya upelelezi Tanzaniaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Eiko Kimura.pdf
Size:
60.17 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: