Dhima ya semi za kawa katika jamii ya watu wa pwani

Date

2016

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Abstract

Semi ni kauli au tungo fupifupi zenye mafunzo na misemo yenye kutoa mafunzo ambayo huonesha mwelekeo Fulani wa maisha. Utafiti huu umechunguza dhima ya semi zilizoandikwa kwenye makawa katika jamii la Dar es salaam na wilaya ya Kilwa. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikua ni kbainisha mitindoya lugha, dhamira na dhima za semi za kwenye makawa. Mbinu za utafiti zilizotumika katika ukusanyaji wa wa data ni ushuhudiaji, usaili na kupitia nyaraka maktabani. Vifaa vilivyotumika katika ukusanyaji wa data ni kamera, simu, kompyuta, karamu na karatasi. Nadharia ya mwitiko wa msomaji na nadharia ya sosholojia zilitumika katika kukamilisha malengo ya utafiti huu. Nadharia ya mwitiko wa msomaji ilitumika zaidi kwa watumiaji wa makawa, watengenezaji , wauzaji, wachoraji na waandishi wa semi za kwenye makawa. Nadharia ya Sosholojia ilitumika kwa sababu semi nyingi zilikuwa zinahusu masuala ya kijmii kama vile mapenzi na upendo, nafsi ya mwanamke katika jamii na kadhalika. Kwa kiasi kikubwa matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti na hivyo kukamilisha malengo ya utafiti, kwani yalibaini kuwa semi za kwenye makawa zimejaa matumizi mbalimabli ya lugha na dhamira. Pia utafiti umebaini kuwa semi za kwenye makawa zina mchango mkubwa katika maisha ya kila siku ya mwanajimii. Huelimisha, kuburudisha na kuonya jamii kuhusu mabbo mbalimbali yaliyopo na yanayotokea katika jamii.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8703.J63)

Keywords

Swahili language, Terms and phrases, Coastal people

Citation

John, S.M (2016) Dhima ya semi za kawa katika jamii ya watu wa pwani, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.