Toni katika vitenzi vya kihehe

dc.contributor.authorElither, Kindole,
dc.date.accessioned2020-04-01T11:31:00Z
dc.date.available2020-04-01T11:31:00Z
dc.date.issued2012
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THSEAFPL8025.T34K56)en_US
dc.description.abstractTasinifu hii ni zao la utafiti ulioshughulikia “Toni katika Vitenzi vya Kihehe”. Kwa ujumla ripoti ya utafiti huu imegawanyika katika sehemu kuu tano ambazo tumeziita sura. Sura ya kwanza imeshugulikia utangulizi kwa ujumla ambapo imeangalia kwa ufupi lugha ya Kihehe, tatizo la utafiti, mapitio ya kazi zilizotangulia na kiunzi cha nadharia kilichotumika katika uchanganuzi wa data ambacho ni Fonolojia Vipandesauti Huru. Sehemu hii pia imetoa maelezo ya mbinu na zana zilizotumika kukusanya data. Aidha, tumeeleza mawanda ya utafiti huu katika sehemu hii. Sura ya pili imeangazia vipengele muhimu vya kiisimu vya lugha ya Kihehe, kama vile vitamkwa na michakato ya kifonolojia na michakato ya kimofolojia. Vilevile sehemu hii imejadili mambo ya msingi kuhusu toni ya lugha ya Kihehe: miongoni mwa mambo hayo ni kiinitoni, kiimbo toni msingi, upachikaji wa kiinitoni na toni inayohusishwa na kiinitoni. Sura ya tatu imejikita zaidi katika uchanganuzi wa data, ambao umeeleza ruwaza ya toni katika vitenzi vya lugha hii. Uchanganuzi ulioibua mchango na mawazo mapya ya utafiti. Sura ya nne imetumika kutoa muhtasari wa tasinifu nzima, hitimisho na mapendekezo kwa ajili ya utafiti zaidi.en_US
dc.identifier.citationElither, K (2012) Toni katika vitenzi vya kihehe, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaamen_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/8714
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaam,en_US
dc.subjectHehe languageen_US
dc.subject, Bantu languageen_US
dc.subjectIringa regionen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleToni katika vitenzi vya kiheheen_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Kindole, Elither.pdf
Size:
98.76 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: