Mkabala wa Kibwege katika fasihi ya Kiswahili Mifano Kutoka Tamthilia ya Amezidi (1995) Said A. Mohamed
dc.contributor.author | Daniel, Zawadi Limbe | |
dc.date.accessioned | 2019-07-30T07:15:57Z | |
dc.date.accessioned | 2020-01-07T16:26:39Z | |
dc.date.available | 2019-07-30T07:15:57Z | |
dc.date.available | 2020-01-07T16:26:39Z | |
dc.date.issued | 2012 | |
dc.description | Available in print form | en_US |
dc.description.abstract | Fasihi ya Kiswahili imepita katika mikabala mbalimbali, mkabala wa Kibwege1 ni mojawapo ya ikabala hiyo. Mkabala huu unaelezwa kuibuka baada ya vita vya pili vya dunia huko Ulaya ambapo, inadaiwa kuwa kuibuka kwake kulitokana na kukata tamaa kwa watu baada ya ugumu wa maisha ulijotokeza mara baada ya kumalizika kwa vita hivyo. Wilson na Alvin (1991) Mkabala huu unatajwa na baadhi ya wahakiki kujitokeza katika tamthilia ya Kiswahili hususan ile ya mwandishi Said A. Mohamed. Huyu ni mwandishi aliyebobea katika utunzi wa kazi za fasihi, hususan tamthilia, riwaya, hadithi fupi na ushairi. Baadhi ya tamthilia zake ni Pungwa (1988), Kivuli Kinaishi (1990), Amezidi (1995), Kitumbua Kimeingia Mchanga (2000), na Posa za Bi Kisiwa (2007). Amezidi (1995) ni moja kati ya tamthilia zenye mtindo wa kipekee katika fasihi ya Kiswahili. Wahakiki wa kazi za fasihi ya Kiswahili kama vile Wamitila (2003), na Njogu na Chimerah (2008) wameitaja tamthilia hii kuwa ni miongoni mwa tamthilia za Kiswahili za mkabala wa Kibwege. Tasnifu hii imechambua na kubainisha sifa na vipengele vya fasihi ya Kibwege na namna vinavyojitokeza katika tamthilia hii ya Amezidi. Aidha, inaeleza namna muktadha wa Tanzania baada ya uhuru ulivyochangia kuibuka kwa thieta ya Kibwege katika fasihi ya Kiswahili. Katika tasnifu hii muktadha unaojadiliwa ni ule wa kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisanaa. Vilevile, nafasi na mchango wa matumizi ya mkabala huu katika fasihi ya Kiswahili vyote vinajadiliwa katika tasnifu hii. | en_US |
dc.identifier.citation | Daniel, Z.L (2012), Mkabala wa Kibwege katika fasihi ya Kiswahili Mifano Kutoka Tamthilia ya Amezidi (1995) Said A. Mohamed, master dissertation, University of Dar es Salaam available at ( ) | en_US |
dc.identifier.uri | http://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3434 | |
dc.language.iso | en | en_US |
dc.publisher | University of Dar es Salaam | en_US |
dc.subject | Swahili literature | en_US |
dc.subject | Mohamed,Said A, Amezidi (1995) | en_US |
dc.title | Mkabala wa Kibwege katika fasihi ya Kiswahili Mifano Kutoka Tamthilia ya Amezidi (1995) Said A. Mohamed | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |