Sayansi katika riwaya ya upelelezi ya kiswahili
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti tuliofanya umelenga kuchunguza sayansi katika riwaya ya upelelezi ya Kiswahili na umeongozwa na nadharia ya muingiliano matini. Tasnifu imejengwa na sura tano ikijaribu kujadili hoja kuwa riwaya ya kisasa ya Kiswahili ina dalili ya kufumbata sifa za kisayansi. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa sayansi imejitokeza kupitia mbinu za kisayansi za utatuzi wa tatizo, mbinu ya saikolojia, mbinu ya isimu ambayo ni sayansi ya lugha na mbinu ya uandishi ya uwekaji kumbukumbu. Utafiti umetusaidia kugundua kuwa sayansi haitajwi wazi na mwandishi au mhusika kuwa sasa hapa sayansi inatumika. Mara chache sana kiashiria cha sayansi hutajwa mfano, saikolojia katika riwaya ya Kosa la Bwana Msa lakini hakikuvishwa hadhi ya kusema ni sayansi. Tumegundua pia kuwa, sayansi hujenga fani kwa kupitia vipengele vya muundo, wahusika na lugha ijengwayo na maneno. Muundo wa moja kwa moja huundwa wakati wa utatuzi wa tatizo hata kama usimuliaji wa hadithi ni wa urejeshi. Kupitia taaluma ya isimu tawi la mofolojia kipengele cha uundaji wa maneno, majina matatu ya wahusika Bwana Msa, AKAZ na FAMBO yamebuniwa na waandishi. Pia istilahi mpya ya neno ‘duni’ inaundwa kutokana na neno ‘dunia’ likiwa na maana tofauti kabisa kupitia mchakato wa udondoshaji. Kimaudhui inafundisha kuwa tupatapo tatizo tuchunguze hatua kwa hatua na kila jambo lina uzuri na ubaya wake kadiri ya lengo la mtumiaji.