Ulinganishaji wa maana za msingi za vidahizo vya Kamusi la Kiswahili ya Bakiza (2010) na kamusi kuu ya Kiswahili ya Bakita (2017)

Loading...
Thumbnail Image
Date
2020
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia ulinganishaji wa maana za msingi za vidahizo vya Kamusi la Kiswahili fasaha ya BAKIZA (2010) na Kamusi Kuu ya Kiswahili ya TUKI (2017). Lengo la utafiti huu ni kubainisha vidahizo vyenye maana za msingi katika kamusi la Kiswahili Fasaha zinazotofautiana na maana za msingi za vidahizo hivyo katika Kamusi Kuu ya Kiswahili na kueleza tofauti zinazojitokeza kati ya maana za msingi za vidahizo vya kamusi la Kiswahili fasaha na maana za msingi za vidohizo hivyo katika kamusi kuu ya Kiswahili. Utafiti huu umefanyyika chuo kikuu cha Dar es salaam na data imekusanywa maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji matini. Uchambuzi wa data umefanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi linganishi na mkabala wa taamuli. Aidha, utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya metaleksikografia iliyoasisiwa na Wiegand (1983) inayofafanua masuala yote ya kileksikografia; kuanzia katika utafiti , ukusanyaji wa data ya Kamusi, uandishi, matumizi na uhakiki wa kamusi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa kuna vidahizo 53 ambavyo maana zake za msingi zinatofautiana katika kamusi teule. Aidha utafiti huu umeeleza tofauti zinazojitokeza kati ya maana za msingi za vidahizo vya kamusi teule. Tofauti hizo ni pamoja na unyume wa maana za msingi, tafauti za mawanda ya maana yam sing (mawanda finyu na mawanda mapana) , uhasishaji na uchanyishaji wa maana za msingi. Matokeo haya yanadhihirisha kuwa kunakutofautiana kwa maana za msingi za vidahizo vya Kamusi la Kiswahili Fasaha na maana za msingi za vidahizo hivyo katika Kamusi Kuu ya Kiswahili. Kutofautiana kwa maana kwa maana za msingi za maneno yaleyale katika lugha moja si jambo la kawaida kwa sababu sifa kuu ya maana ya msingi ni kutokubadilika kulingana na muktadha. Kwa hivyo, ni muhimu kwa wanaleksikografia (waandaaji wa kamusi)) walimu kiswahili, wajifunzaji na wanaisimu kwa ujumla kutambua tofauti hizo za maana za msingi kwa kuwa itawasaidia kutumia lugha kwa uangalifu ili kuleta ufanisi katika mawasiliano na maendeleo ya lugha ya Kiswahili. Pia, tunapendekeza kuwa ikiwa tofauti hizo za maana za msingi zitaendelea kuwepo, waandaaji wa kamusi wanapaswa angalau kueleza katika kamusi zao kwa kuwakamusi hizo (Kamusi la Kiswahili Fasaha na Kamusi Kuu ya Kiswahili) ni za lugha ya Kiswahili kwa ujumla zenye kulenga watumiaji wote wa lugha bila kujali muktadha. Hatimaye tunapendekeza kufanyika kwa tafiti fuatishi ili kuchunguza sababu za kutofautiana kwa maana hizo za msingi katika Kiswahili pamoja na athari zake kwa ujumla.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8701.T34H385)
Keywords
Languages, Swahili languages dictionary, BAKITA, Tanzania
Citation
Haule, J,(2020) Ulinganishaji wa maana za msingi za vidahizo vya Kamusi la Kiswahili ya Bakiza (2010) na kamusi kuu ya Kiswahili ya Bakita (2017), Master dissertation,University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.