Ulinganishi wa methali za lugha mbili katika kamusi thania mifano kutoka kamusi ya Kiswahili – Kiingereza ya TUKI (2014)

Date

2017

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu, ulijihusisha na ulinganishi wa methali za lugha mbili katika Kamusi Thania. Kamusi iliyotumika katika utafiti huu ni Kamusi ya Kiswahili – Kiingereza, Toleo la Pili iliyotungwa na TUKI (2014). Katika ulinganishaji huo methali za Kiswahili na zile za Kiingereza zilizoingizwa katika kamusi hii zilitumika. Mtafiti alitumia mbinu mbalimbali katika kuhakikisha lengo kuu na malengo mahususi ya utafiti huu yanafikiwa. Data ya utafiti huu ilikusanywa kutoka maktabani na uwandani. Katika kukusanya data za uwandani mtafiti alitumia mbinu za hojaji na mahojiano. Kwa upande wa data za maktabani mtafiti alifanya uchunguzi na uchambuzi wa methali mbalimbali kupitia Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza, Toleo la Pili ya TUKI (2014). Katika kuzichambua data hizo, mtafiti alitumia mkabala wa maelezo kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, mkabala wa kiidadi ulitumika pale palipohitajika. Nadharia ya Maana ni Matumizi ilitumika katika kuchambua data zinazohusiana na ulinganishaji wa taswira na maana za methali hizi. Matokeo ya utafiti huu kwa ujumla yaliweza kutupatia makundi mawili ya methali. Kundi la kwanza ni la methali zinazofanana taswira na maana na kundi la pili ni lile la methali zinazotofautiana taswira lakini zinafanana maana. Pia, sababu mbalimbali zilizopelekea kufanana na kutofautiana kwa taswira na maana katika methali hizo zimefafanuliwa. Kutokana na matokeo ya utafiti, mtafiti anapendekeza zifanyike tafiti zaidi zinazohusiana na ulinganifu wa methali za lugha mbili zilizoingizwa katika kamusi thania mbalimbali ili kuweza kubaini kufanana na kutofautiana kwa methali hizo katika vipengele tofauti vya lugha.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PN6515.S9A222)

Keywords

Proverbs, swahili, Proverbs, English

Citation

Abdalla, K.J. (2017) Ulinganishi wa methali za lugha mbili katika kamusi thania mifano kutoka kamusi ya Kiswahili – Kiingereza ya TUKI (2014). Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.