Muundo wa kirainomino katika lugha ya Kihehe
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu ulihusu muundo wa kirainomino (kwa hiyo, KN) katika lugha ya Kihehe, ambayo huzungumzwa mkoa wa Iringa katika wilaya za Iringa, Mufindi na Kilolo. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza muundo wa kirainomino katika lugha ya Kihehe. Utafiti umefanyika katika vijiji vya Wasa, Usengelindete, Ihomasa na Ufyambe katika kata ya Wasa, wilaya ya Iringa mkoa wa Iringa, Tanzania. Ili kukamilisha kazi hii, Nadharia ya Msingi wa Isimu iliongoza utafiti huu, yaani ufafanuzi wa vipengele mbalimbali vya lugha huzingatia jinsi wazungumzaji wa lugha husika wanavyozungumza lugha yao na si kwa kuongozwa na kanuni za lugha za Ulaya. Mbinu za utafiti zilihusu: muundo wa utafiti, eneo la utafiti, sampuli ya watafitiwa, ukusanyaji, uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Data ya utafiti ni ya aina mbili, yaani data ya msingi na data fuatizi ambapo miundo mbalimbali ya tungo ilikusanywa na kuchambuliwa ili kuchunguza muundo wa KN katika lugha ya Kihehe. Kazi imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza, imeeleza kiini cha utafiti na utaratibu uliozingatiwa katika kufanikisha utafiti. Sura ya pili, imeshughulikia mapitio ya maandiko kuhusiana na muundo wa KN katika lugha za Ulaya na katika lugha za Kibantu. Mapitio haya, yamebainisha kuwa kuna tofauti ya muundo wa virainomino katika lugha za ulaya na zile za Kibantu. Aidha, mpangilio wa viandami vya KN hutofautiana kati ya lugha moja na nyingine. Sura ya tatu, imehusu mbinu za utafiti. Sura ya nne, imeshughulikia uchanganuzi wa data. Kwa ujumla, data iliyopatikana imechanganuliwa kwa njia ya maelezo. Nadharia ya msingi wa Isimu ya Dixon (1997) iliongoza mjadala na uchanganuzi wa data hii. Sura ya tano imeshughlikia muhtasari, matokeo na mapendekezo kwa tafiti nyingine. Matokeo ya utafiti yamebainisha vijenzi nane(8) vy KN cha Kihehe. Kimpangilio, KN cha Kihehe huanza na neno kuu na viandami vingine hufuata neno kuu. Hii ina maana kuwa kanuni ya jumla aliyoitoa rugemalira (2007) kuhusu mpangilio wa KN katika lugha za kibantu, inapingana na utafiti huu. Katika mazungumzo ya kawaida, miundo mingi huwa na viandami hadi vine. Lakini miundo mirefu huwa na viandami hadi tisa. Kuhusu dhima za KN cha Kihehe, ni kiima cha sentensi, yambwa na yambiwa. Pia, KN huwa na dhima