Haja ya kuunda kamusi ya majina ya watu ya asili: majina ya asili katika jamii ya Wahaya

Date

2011

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu unahusu haja ya kuunda kamusi ya majina ya watu ya asili katika jamii lugha ya Wahaya nchini Tanzania. Haja ya kuunda kamusi imetokana na ukweli kuwa kamusi nyingi zimeweka kando uingizaji wa majina ya watu katika kamusi kama sehemu ya msamiati wa lugha hizo isipokuwa kama majina hayo ni ya watu maarufu au majina maaluma kama vile ya pacha. Hivyo mtafiti amekusanya majina ya watu ya asili kutoka jamii lugha ya Wahaya na kuyatolea maana kikamusi pamoja na kuchunguza sababu inayosukuma mhusika kupewa jina husika ili kubaini kama yanatolewa kiholela au la. Utafiti huu umehusisha sura tano, Sura ya kwanza ina utangulizi unaojihusisha na usuli wa tatizo, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, na mawanda ya utafiti. Sura ya pili inahusika na machapisho ya vitabu na kiunzi cha nadharia ambayo Nadharia ya Uumbaji (mould theory) ndiyo imetumika kama mhimili wa utafiti huu. Sura ya tatu imehusika na mbinu na njia za utafiti zilizotumika kufanikisha utafiti huu. Mbinu zilizo tumika ni mbinu ya maktabani ambapo nyaraka za maktabani zenye utafiti wa majina ya watu ya jamii hii zimekusanywa ili kupata taarifa za utafiti huu. Njia ya mahojiano, na njia ya hojaji zimetumika katika kupata data za utafiti.Sura ya nne imehusika na uwasilishaji, uchambuzi, ujadilifu wa data za utafiti kama zilivyopatikana kutoka uwandani; data zimegawanyika katika sehemu mbili, ambapo sehemu ya kwanza inahusu sababu zinazomsukuma mtu kupewa jina husika ambazo zimeainishwa katika makundi manne, na sehemu ya pili ni ile inayohusu muundo wa kamusi ya majina ya watu ya asili ya jamiilugha ya Wahaya. Sura tano na ya mwisho katika utafiti huu, imehusika na majumuhisho, hitimisho, na mapendekezo.

Description

Available in print

Keywords

Haya language, Names, Haya, Dictionaries

Citation

Salapion, D (2011) Haja ya kuunda kamusi ya majina ya watu ya asili: majina ya asili katika jamii ya Wahaya. Tasinifu ya M. A. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx