Usawiri wa mhusika mwanamke katika ushairi wa Mathias Mnyampala: mifano kutoka diwani ya Mnyampala (1965) na waadhi wa ushairi (1965)
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza namna mwanamke alivyosawiriwa katika Diwani ya Mnyampala (1965) na Waadhi wa Ushairi (1965). Kazi hii iliongozwa na malengo matatu: Kwanza, kubainisha namna mwanamke alivyosawiriwa katika hizi mbili. Pili, kuchunguza muktadha uliomsukuma mwandishi kumsawiri mwanamke kwa namna alivyomsawiri katika vitabu hivi. Tatu, kuchambua dhima ya usawiri huo katika kipindi cha Mnyampala na baadaye. Katika utafiti wetu tulitumia mbinu za maktabani na uwandani ambapo vifaa kama vile kalamu, karatasi (shajara) na kompyuta vilitumika katika ukusanyaji wa data zilizohitajika. Aidha, tulifanya mahojiano na baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili katika vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma. Nadharia ya Ufeministi na mkabala wa kimaelezo viliongoza uchambuzi wa data zilizopatikana katika utafiti huu. Matokeo ya uchambuzi yalibainisha kuwa mwanamke amesawiriwa katika mtazamo chanya na hasi. Pia, ilibainika kuwa miktadha ya kijamii, kiuchumi, mwingiliano matini, mahusiano binafsi, wakati na mahali ndio iliyoibua usawiri wa mwanamke katika diwani teule. Aidha, dhima ya usawiri huo ilibainika kuwa ni pamoja na kufunza, kuonya, kukosoa, kuhamasisha na kuzindua jamii kupitia masuala mbalimbali yanayomhusu mwanamke. Pia, utafiti huu umewashauri wasanii kutumia kalamu na kazi zao kumzungumzia mwanamke katika namna itakayochochea ukombozi wa mwanamke na ustawi wa mwanamke na jamii yake kwa ujumla.