Tathmini ya kufahamika kwa lugha Kienzo ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI, 2013) kwa walimu na wanafunzi wa sekondari

Date

2016

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu umehusu lugha kienzo ya kamusi. Lengu kuu la utafiti lilikuwa kutathmini kufahamika kwa lugha ya kienzo ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Tatu (TUKI, 2013) miongoni mwa walimu na wanfunzi wa sekondari . Malengo mengini mahususi yalikuwa; (i) kuhakiki kiwango wa ufundishwaji wa mada ya lugha kienzo ya kamusi katika shule za sekondari, (ii) kufafanua weledi wa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari katika lugha kienzo ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI, 2013) na (iii) kujadili changamoto zinazowakabili walimu na wanafunzi kutokana na lugha kienzo ya kamusi na namna ya kukabiliana na changamoto hizo. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka uwandani na maktabani. Katika utafiti wa maktabani, tulikusanya data za awali na fuatizi kwa kusoma matini na nyaraka zilizohusiana na utafiti huu kama vile Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI, 2013) na kazi za watafiti mbalimbali waliowahi kutafiti suala la lugha kienzo ya Kamusi. Kwa upande wa utafiti wa uwandani mbinu za hojaji na mahojiano zilitumika kukusanya data za utafiti huu kutoka kwa alimu walimu na wanafunzi wa shule za sekondari. Data zilizokusanywa zilichambuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia njia ya maelezo na takwimu. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Maana kama matumizi iliyoasisiwa na Wittgenstein (1953). Nadharia hii inaeleze kwamba, ni kosa kuweka mipaka ya maana kama ambavyo nadharia za maana kama dhana na maana kama kitajwa zinavyoelezwa. Kwa kufanya hivyo ni sawa na kuweka mipaka ya thamani ya umbo lenyewe la kiisimu. Kinachopaswa kuzingatiwa ni matumizi ya maneno au matumizi ya maumbo ya kiisimu au vitajwa. Hivyo, ni lazima kuangalia maneno au maumbo ya kiisimu yametumikaje. Haina haja ya kuuliza neno hili lina maana gani bali limetumikaje. Nadharia ya maana kama matumizi ilitufaa katika kuchambua data za utafiti ulizohusu lugha kienzo ya kamusi kwa kuwa inazingatia maana ya umbo la kiisimu katika lugha na matumizi yake. Hili ni kutokana na ukweli kwamba tarakimu, vifupisho na alama zina maana tofauti na ile maana inayopatikana katika muktadha wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI, 2013). Matokeo ya utafiti huu yananaonesha kuwa, lugha kienzo ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2013) haifundishwi kikamilifu katika shule za sekondari. Hivyo, kutofahamika kwa lugha kienzo ya kamusi hii ni kwa walimu na wanafunzi inasababisha wakose maarifa yaliyofumbatwa na luga hiyo katika kamusi husika. Kwa, hiyo tunapendekeza kwamba ipo haja ya kufundisha mada ya luga kienzo ya kamusi ili kuwawezesha wanafunzi kupata stadi za kutumia kamusi. Pia, walimu wapewe mafunzo ya kutosha kuhusu taaluma ya leksikografia. Vilevile, walimu wa sekondari wawe wabunifu na washiriki katika shughuli za kileksikografia kama vile, kuunda na kuhariri kamusi.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8703.M85)

Keywords

Swahili language, Dictionaries, Swahili, High school students, High school teachers

Citation

Mwinuka, Y (2016) Tathmini ya kufahamika kwa lugha Kienzo ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI, 2013) kwa walimu na wanafunzi wa sekondari, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.