uhusiano wa taashira na maisha ya shujaa wa kiutendi: uchunguzi wa utenzi wa rasi ‘lGhuli (1979) na utenzi wa Nyakiiru Kibi (1997)

Date

2017

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu kuhusu uhusiano wa taashira na maisha ya shujaa katika Utenzi wa Rasi ‘lGhuli (1979) na Utenzi wa Nyakiiru Kibi (1997) ulikuwa na malengo matatu ambayo ni: kubainisha taashira zinazotumika katika tendi teule; kueleza uhusiano wa taashira hizo na maisha ya mashujaa wa tendi teule; na, kufafanua dhima ya matumizi ya taashira katika ujenzi wa shujaa katika tendi za Kiswahili. Ili kutimiza malengo hayo, data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia njia kuu tatu (3) ambazo ni: ukusanyaji matini, udurusu matini na uchambuzi matini. Aidha, ufasili wa data uliongozwa na Nadharia ya Semiotiki na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji. Kuhusu matokeo ya utafiti, imebainika kwamba tendi teule zimetumia idadi tofautitofauti za taashira. Vilevile, imebainika kuwa taashira zinazotumika katika tendi andishi za Kiswahili ni za aina mbalimbali ambazo zinajumuisha: taashira za wanyama, mandhari au mazingira asilia, wahusika au majina, wadudu, ndege, mavazi, vifaa utamaduni) pamoja na taashira za kimatendo au kimatukio. Kuhusu uhusiano baina ya taashira na maisha ya mashujaa, ilibainika kwamba matumizi ya taashira katika tendi yana uhusiano mkubwa na maisha ya mashujaa. Uhusiano huo umebainika kujidhihirisha kupitia sifa za jumla za mashujaa wa utendi; imani za mashujaa wa utendi; mahusiano baina ya mashujaa wa tendi na jamii zao; na, mafanikio, anguko pamoja na hatima ya shujaa. Mwisho, imebainika katika utafiti huu kwamba matumizi ya taashira katika tendi za Kiswahili yana dhima kubwa sana katika ujenzi wa mashujaa. Baadhi ya dhima hizo ni kama vile: kueleza na kufafanua maisha ya shujaa wa kiutendi, kueleza uhalisia wa shujaa husika, maisha yake, tamaduni na jamii inayomjenga shujaa huyo. Kuhusu maeneo yanayohitaji tafiti fuatizi, utafiti huu unapendekeza kufanyika kwa tafiti za kina katika vipengele vingine vya tamathali za semi na dhima zake katika tendi, uhusiano wa taashira na tendi nyingine simulizi pamoja na kuchunguza kuhusu shujaa wa kihistoria yaani, shujaa halisi katika tendi za Kiswahili.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.M7833)

Keywords

Swahili poetry, Symbolism in literature, Utenzi wa Rasi Ighuli (1979), Utenzi wa Nyakiiru kibi (1997)

Citation

Mtega, W. (2017) uhusiano wa taashira na maisha ya shujaa wa kiutendi: uchunguzi wa utenzi wa rasi ‘lGhuli (1979) na utenzi wa Nyakiiru Kibi (1997). Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.