Mhusika zimwi na jini katika ngano za Kiswahili: uchambuzi linganishi wa dhima yao kimaudhui

Date

2016

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu unahusu kulinganisha dhima za mhusika Zimwi na Jini kimaudhui katika ngano za Kiswahili. Utafiti huu ulikuwa na malengo ya kubainisha uhusika wa Zimwi na Jini katika ngano teule za Kiswahili. kuchambua dhima ya kimaudhui ya mhusika Zimwi na Jini na kulinganisha dhima za kimaudhui za wahusika hao katika ngano teule za Kiswahili. Katika kukusanya na kuchambua data tumetumia ngano teule na marejeleo mbalimbali kutoka maktabani. Mbinu ya uchambuzi wa matini, mkabala linganishi na nadharia ya naratolojia zimetumika katika utafiti huu kumsaidia mtafiti kutimiza malengo ya utafiti. Katika utafiti huu tumebaini kuwa dhima za mhusika Zimwi na Jini katika ngano teule za Kiswahili ni kuibua dhamira mbalimbali kama wivu na tamaa, upumbavu na ujinga, ujasiri na ushujaa, mapenzi, mgongano wa wema dhidi ya ubaya na uzalendo. Pia mitazamo na migogoro mbalimbali imejadiliwa iliyoibua dhamira nyingine. Aidha wahusika mazimwi na majini pia yamesaidia kuonesha misako mbalimbali iliyozifanya hadithi kuwa endelevu. Kwa ujumla kuwapo kwa mazimwi na majini katika hadithi hizi kumesaidia kuendeleza hadithi hatimaye kufikia kileleni. Pia katika ulinganishi wa mhusika Zimwi na Jini, mazimwi na majini yametokea kufanana katika dhima zao. Kwa kuwa wote wana dhima sawa za kimaudhui. Mazimwi na majini, yote kwa pamoja yameweza kuibua dhamira, kujenga na kuendeleza ngano hadi kufikia tamati na hata kuonyesha usawa katika mgongano wa wema dhidi ya uovu. Hivyo matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa dhima za mhusika Zimwi na Jini kimaudhui zinafanana.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.5.L46)

Keywords

Swahili language

Citation

Leonard, M. (2016) Mhusika zimwi na jini katika ngano za Kiswahili: uchambuzi linganishi wa dhima yao kimaudhui, Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu ch Dar es Salam, Dar es Salaam